March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Sura mpya 10 zaibuka kidedea kura za maoni CCM Tabora

Na Allan Kitwe, Timesmajira Online -Tabora

Zoezi la upigaji kura za maoni kwa watia nia wa nafasi ya Ubunge na Udiwani ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),ngazi ya Kata na na majimbo,limehitimishwa jana na kushuhudiwa sura mpya zikipenya katika uchaguzi huo.

Akizungumza na gazeti hili Agosti 5,2025,Katibu wa Siasa na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tabora Idd Moshi,ameeleza kuwa zoezi hilo limefanyika kwa amani na utulivu katika Wilaya zote za Mkoa huo.

Amebainisha kuwa katika majimbo 12 yaliyopo katika Mkoa huo ni majimbo mawili tu ambayo Wabunge wanaomaliza muda wao wamepata ushindi katika hatua hiyo ya kura za maoni.

Ametaja majimbo 2 ambayo wabunge wa zamani wamepeta kuwa ni Urambo Magreth Sitta na Nzega Mjini Hussein Bashe huku majimbo 10 yaliyobaki walioshinda kura za maoni ni sura mpya.

Ametaja walioibuka kidedea katika jimbo la Tabora Mjini ni Shabani Mrutu, Uyui ni Shaffin Sumar,Sikonge ni Munde Tamwe, Kaliua Denis Kilatu na Bukene ni John Luhende).

Majimbo mengine ni Nzega Vijijini ambapo aliyeibuka kidedea ni Neto Kapalata, Manonga ni Abubakar Omari, Igunga Mjini ni Henry Kabeho,Igalula ni Juma Kawambwa na Ulyankulu-Kaliua ni Japhael Lufungija.

Moshi,amefafanua kuwa haya ni matokeo ya awali ambayo yatapelekwa katika vikao vya ngazi za juu ya chama kwa ajili ya uteuzi wa mwisho, aliwataka wagombea wote kuwa watulivu na kusubiri uamuzi wa vikao.