Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online
Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inayodhaminiwe na bia ye Serengeti inaingia kambini leo, kujiandaa na mechi ya kirafiki ya Kalenda ya FIFA itakayochezwa Oktoba 11 mwaka huu kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Wachezajl walloitwa na kocha wa timu ya Taifa ya Taifa ya Tanzania Etienne Ndayiragije wameanza kuripoti Kambini.
Hata hivyo, nahodha wa timu hiyo Mbwana Samatta anatarajia kuwasili kesho Jumanne alfajiri akitokea Uturuki wakati Thomas Ulimwengu akiwasili leo mchana kutokea DR Congo.
Mchezaji Himid Mao atawasili keshokutwa Jumatano asubuhi akitokea Misri, Simon Msuva, Nickson Kibabage wataingia Jumatano usiku kutoka Morocco na Ally Msengi tayari amewasili kutokea Afrika Kusini.
%%%%%%%%%%%%%
More Stories
Zanzibar kuzalisha wachezaji wenye vipaji
Othman awakabidhi jezi Zanzibar Heroes
Rais Samia: Yanga endeleeni kuipeperusha bendera ya Tanzania