Na Penina Malundo,Timesmajira
BENKI ya Stanbic imesema kuwa itaendelea kushirikiana na Makampuni ya madogo ya Kitanzania yanayojishughulisha na uchimbaji wa mafuta na gesi katika kuwapa uzoefu katika miradi mikubwa ijayo.
Akizungumza hayo jana katika Kongamano na maonesho ya Petroli ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAPCE’25),Makamu wa Rais wa Miundombinu ya Nishati,Joe Mwakenjuki amesema wameona makampuni ya watanzania yakijitokeza katika kuangalia fursa mbalimbali katika miradi ya mafuta na gesi.
Amesema benki ya Stanbic imeweza kusaidia makampuni hayo madogo ya kizalendo katika mnyororo wa thamani kwenye shughuli zao za mafuta na gesi.
“Benki yetu imekuwa mstari wa mbele katika kusaidia Kampuni ndogo za kitanzania katika kuwapa uzoefu katika miradi yao ya sasa wanayofanya ambayo ni midogo.
” Ni vema wenyewe kujipa uzoefu katika miradi ya sasa na sio kusubiri miradi mikubwa ya mafuta na gesi kufanya hata hii midogo wanaweza kufanya,”amesema.
Amesema watanzania wajitokeza kwa wingi katika kuchangamkia fursa za miradi ya mafuta na gesi na kujiandaa na miradi mikubwa zaidi kuliko wanayotekelezwa kwa sasa.
“Wanaweza kuja katika mabenki na kuweza kuwasaidia kupata uzoefu ili miradi mikubwa inapokuja tutaweza kuwasaidia zaidi kwani mahitaji ya kifedha,amesisitiza.
More Stories
Askofu Masondole awataka vijana kutofuata mila na desturi zisizokubalika nchini
Dkt.Samia azindua jengo la Makao Makuu ya Mahakama,ataka kasi ya utoaji haki iendane na ubora wa jengo hilo
Dkt.Biteko :Mradi wa Kufua umeme wa JNHPP wakamilika rasmi