Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma.
SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Tulia Ackson amelitaka Shirika la Posta Tanzania kuongeza juhudi zaidi katika huduma zao kwasababu suala la anuani za makazi limeboreshwa zaidi.
Amesema kuboreshwa kwa suala la anuani za makazi kunalifanya shirika la posta kuwa na kazi zaidi za kupeleka mizigo ya wateja hadi nyumbani kwa kutumia anuani za makazi.
Dkt.Tulia ametoa agizo hilo jijini hapa,alipokuwa anatembelea mabanda ya maonesho ya taasisi zinazohusiana na Wizara ya habari, mawasiliano na Teknolojia ya Habari kuelekea uwasilishaji wa bajeti ya wizara hiyo.
Ameeleza kuwa kuwepo kwa mfumo wa anuani za makazi kunasaidia Kwa kiasi kikubwa Shirika hilo ,kuwafikia wateja endapo mteja atakuwa amesajili makazi yake hivyo kumuwezesha mtoa huduma wa Posta kufahamu Kwa haraka namba ya nyumba, jina la mtaa au Barabara, pindi anapopeleka mzigo Kwa mteja wake hivyo ni vyema kuongeza nguvu zaidi.
“Shirika letu la posta sasa nafikiri mjipambanue zaidi Kwa sababu mmewezeshwa Kwa kiasi kikubwa na zoezi la anuani ya makazi ukimutumia mtu barua inaenda hadi nyumbani kwake kwakuwa tayari namba ya nyumba yake inafahamika hivyo ongezeni nguvu,
“Nimefurahi sana nimeona zoezi hili la anuani za makazi ambayo yameanza mapema mwaka Jana na sasa tumefikia mahali ambapo yule aliyesajili anuani yake anaweza kuipata kiganjani Kwa kutumia aina yeyote Ile ya Simu kwahivyo nichukue fursa hii kuwapongeza wizara,.mtu kujua anuani yake ni muhimu sana na wale Wananchiwenzangu ambao hamujajisajili mjisajili muweze kupata huduma Kwa haraka,”amesema Tulia.
Kwa upande wake Mkuu wa Mawasiliano na mambo ya Posta, Kimataifa Elia Madulesi amesema kuwa anuani za makazi zimewezesha kuwafikia wateja wao hadi majumbani hivyo kwao ni jambo kubwa sana ambapo linapunguza muda wa mwananchi kufikia ofisini.
Kutokana na hayo amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuweka msisitizo Kuwafikia wananchi Kwa huduma mbalimbali kwani Shirika la posta wanazo anuani za makazi ambazo mfumo wake upo tayari wanaoweza kutumia katika huduma mbalimbali katika kutoa huduma ikiwemo huduma ya vifurushi ambapo wanafika popote.
” Tunasema tunakufikiia popote ulipo sababu anuani Inatuwezesha kufika ulipo hivyo Mwananchi haitaji tena kututafuta sisi ndio tunakufuata popote pale ulipo”amesema Madulesi .
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa