November 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

PMO 0150 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapteni Mstaafu, George Mkuchika (kushoto) baada ya Bunge kupitisha Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Taasisi zake na Mfuko wa Bunge kwa mwaka 2020/2021. Wa tatu kulia ni Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Dkt. Augustine Mahiga, kulia ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia , Profesa Joyce Ndalichako, na wa pili kulia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt Angelina Mabula. (Picha na OWM)

Spika Ndugai aweka hadharani mamilioni aliyolipwa Lissu

Na Mwandishi Wetu

SPIKA wa Bunge, Job Ndugai, amefunguka kuhusu kile ambacho aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki kwa tiketi wa CHADEMA, Tundu Lissu, amelipwa kwa kindi alichokuwa mbunge na kupinga madai yanayotolewa na mwanasiasa huyo kwamba bado anadai.

Kauli hiyo ya Ndugai imekuja siku chache baada ya Lissu kunukuliwa na chombo kimoja cha habari akisema madai ya Spika kuwa amelipwa na hakuna anachodai ni uongo.

Akizungumza Bungeni jijini Dodoma wakati akiahirisha Bunge, Spika Ndugai alihoji; “Hivi ni nani humu hakuwahi kupata mshahara? Mishahara yote (Lissu) tangu ameanza ni zaidi ya sh. milioni 200 ambazo tumemlipa. Wakati mwingine mtu uwe na shukrani hapa duniani.”

Kwa upande wa posho, Spika Ndigai alisema Lissu amelipwa zaidi ya sh. milioni 360. “Na zilikuwa zinapita wapi kama si kwa Ndugai, kwa ujumla amelipwa zaidi ya milioni 500, sitaki kutaja zaidi, akitaka twende nitafunguka,”alisema.

Alisema Lissu ana mikopo ambayo amechukua zaidi ya milioni 70 alizokopa. “Huko aliko awe analeta hela kwa ajili ya kulipa mikopo. Sio utamaduni wetu kuweka mambo ya mtu hadharani, lakini inapotokea kwenye mitandao akadai mambo ambayo hayana kichwa na miguu haipendezi,”alisema.

“Mheshimiwa Tundu Lissu akumbuke kuna posho ambazo tumekuwa tukilipa dereva kwenda wapi,pesa za jimbo umelitembelea wapi na lini? Kwa hiyo wewe huyo huyo unaweza kujikuta huko kwenye balaa la kutakiwa kurudisha hizo fedha,” alisema na kuongezal;

“Bahati mbaya huko aliko Ubelgiji Corona ni hatari, kaa ndani au urudi huku mwezi wa 10 ngome iko uwanjani.”

Alifafanua kwamba kwa wabunge wote kufikia Juni 30, mwaka huu hesabu zake zitakuwa tayari, kila mbunge atakuwa anaelewa anadai nini, amelipwa nini na hata walio mahakamani.

“Na wabunge wengi kama wana hela ni kidogo sana., madeni ni mengi sana ni vema kila mtu akapiga mahesabu yake vizuri. Sio tunaangalia bajeti ya Waziri Mipango na kuikosoa, sasa na ninyi lazima mjiangalie kwani kudaiwa sana zaidi ya mapato yako ni moja ya kukosa kuwa kiongozi,” alisema.

Aliwakumbusha wabunge wenye madeni kulipa madeni yao. “Kuna faili watu wamekopa bila aibu kama sio viongozi, kwa wapiga wao, kwenye SACCOS na kwenye mabenki,” alisema.