Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Balozi Willibrod Slaa ameunga mkono uwekezaji kwenye Bandari ya Dar es Salaam, lakini ameishauri Serikali kurekebisha kasoro zinazolalamikiwa kwenye mkataba wa uwekezaji na kampuni ya DP World ya Dubai.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Slaa amesema kuwa mikataba ya nchi hodhi (host government agreement) na mikataba kati ya nchi na nchi (intergovernmental agreement) kama uliopitishwa juzi na Azimio la Bunge siyo jambo la kigeni.
“Dosari za wazi katika mkataba huu ziondolewe, ili mkataba huu uweze kuendelea katika hatua za awali na iwapo kampuni husika tutaridhika nayo mkataba uongezwe kwa jinsi tutakavyowapima na kwa kila hatua kuzingatia maslahi ya usalama wa taifa letu,” Slaa aliwaambia waandishi wa habari.
More Stories
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba
TRA kuongeza idadi ya waendesha uchumi walioidhinishwa
TRA Tanga wajivunia ukusanyaji mapato