MADRID, Uhispania
KOCHA wa tletico Madrid Diego Simeone, amejitia kitanzi kuitumikia timu hiyo baada ya kusaini mkataba mpya ambao unatarajiwa kumalizika 2024.
Simeone, mwenye umri wa miaka 51 raia wa Argentina, aliwaasili katika mji mkuu wa Uhispania kama kocha mnamo 2011, na kuiongoza Los Rojiblancos kutwaa mataji nane na hivi karibuni Ubingwa wa La Liga ya msimu uliopita, kitu ambacho Simeone atakuwa na hamu ya kutetea msimu huu unaokuja.
Hata hivyo, Simeone ndiye kocha aliyehudumu kwa muda mrefu zaidi katika historia ya Atletico Madrid na kocha aliyehudumu kwa muda mrefu kwa sasa katika soka la Uhispania.
Makombe nane ambayo ameongoza klabu ni zaidi ya kocha yeyote katika historia ya Rojiblancos; Wakati wa uongozi wake, Atletico wameshinda La Liga, Europa League na Super Cup ya UEFA mara mbili kwa kila moja na Copa del Rey moja na Supercopa de Espana. Pia wamefika fainali ya Ligi ya Mabingwa mara mbili.
Atletico itaanza msimu mpya mnamo Agosti 15 kwa mchezo wa ugenini dhidi ya Celta Vigo. Kisha watawakaribisha Elche huko Wanda Metropolitano katika mchezo wao wa kwanza wa nyumbani msimu wa 2021-22.
More Stories
Samia awazawadi Stars milioni 700/-
Samia atoa bilioni 8/- kukarabati viwanja vya CHAN, AFCON
Rasmi Chatsoko mdhamini mkuu wa Goba Hills Marathon 2025