Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online
MABINGWA mara tatu mfululizo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL), Simba wamefanikiwa kuibuka na ushindi mnono wa goli 6-0 dhidi ya wapinzani wao Vital’O ya Burundi katika mchezo wa kirafiki wa maadhimisho ya siku ya Simba ‘Simba Day’ uliochezwa kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.
Ushindi huo ni wa pili mfululizo kwa Simba katika maadhimisho ya Tamasha hilo baada ya msimu uliopita kupata ushindi wa goli 3-1 mfungani bora kwa misimu miwili mfululizo Meddie Kagere akidhihirisha ubora wake baada ya kufunga goli tatu ‘Hat trick’ dhidi ya wapinzani wao Power Dynamo.
Katika mchezo huo, Simba walianza na kikosi kilichokuwa na mchanganyiko wa wachezaji wapya na wale wa zamani ikiwa ni mpango wa benchi lao ufundi kuangalia ubora wa maandalizi waliyoyfanya toka wakiengie kambini kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao
Morrison alifanikiwa kufungua akaunti ya magoli kwa Simba akifunga goli la kwanza dakika ya 44 akipokea pasi nzuri iliyopigwa na kiungo Mzambia, Rally Bwalya.
Baada ya dakika tatu, Nahodha , John Bocco aqliwainua tena mashabiki wa Simba baada ya kufunga goli la pili akipokea krosi ya Morrison.
Kipindi cha pili, benchi la ufundi la Simba chini ya kocha wake Mbelgiji Sven Vandenbroeck alibadili kikosi kizima ambacho kilikwenda kutanua ushindi hadi mabao matano.
Licha ya mabadiliko hayo kupunguza kasi iliyoonekana katika kipindi cha kwanza lakini wachezaji wa Simba waliendelea kuutawala mchezo huo na dakika ya 56 kiongo bora wa msimu uliopita, Clatous aliifungia simba goli la tatu.
Goli hilo liliongeza kasi ya mashambulizi kwani dakika ya 77, Ibrahim Ajibu alifunga goli la nne dakika ya 76 akimalizia pasi ya Chama, mshambuliaji mpya Chriss Mugalu alifunga goli la tano dakika ya 78 huku Charles Ilamfya akifunga goli la sita dakika ya 90
Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Aishi Manula/Beno Kakolanya dk.46/Ally Salim dk69, Shomari Kapombe/David Kameta dk46, Gardiel Mchael/Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ dk46, Ibrahim Ame/Kennedy Willson dk46, Joash Onyango/Gerson Fraga dk46, Jonas Mkude/Muzamil Yassin dk46, Hassan Dilunga/Ibrahm Ajibu dk46, Rally Bwalya/Clatous Chama dk46, John Bocco/Chris Mugalu dk46, Said Ndemla/Miraj Athuman ‘Madenge’ dk46 na Bernard Morrison/Charles Ilamfya dk46.
More Stories
15 wajinoa Juventus,akiwemo mtoto wa Mwenyekiti wa CCM Mbeya
Za Kwetu Fashion Show, yawapaisha wanamitindo nchini
TCAA yaadhimisha siku ya usafiri wa anga Duniani kwa kushiriki mbio za Marathon UDSM