June 20, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Sillo:Tanzania itakuwa mwenyeji bora AFCON 2027

Na Zena Mohamed,TimesmajiraOline,Dodoma

NAIBU Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Daniel Sillo, amesema Serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali za maandalizi ya michuano ya Africa Cup of Nations (AFCON)2027 ili kuhakikisha Tanzania inakuwa mwenyeji bora wa mashindano hayo.

Sillo amesema hayo jijini hapa leo 20,2026 wakati akizungumza kwenye Bonanza la Bunge(Bunge Grand Bonanza ) ambapo amesema umwekezaji unaoendelea kufanyika katika miundombinu ya michezo pamoja na huduma muhimu utasaidia nchi kuwa tayari kwa kiwango cha juu cha kuandaa michuano hiyo mikubwa ya bara la Afrika.

“Tunaijivunia kuona Tanzania ikiwa miongoni mwa wenyeji wa AFCON 2027. Bunge litaendelea kushirikiana na wadau wote kuhakikisha maandalizi yanafanyika kwa viwango vya juu na kuacha historia nzuri kwa Taifa letu,” amesema Sillo.

Aidha, amesema Bonanza la Bunge (Bunge Grand Bonanza) linaendelea kuwa jukwaa muhimu la kuhamasisha wananchi kufanya mazoezi, kushiriki michezo na kuimarisha mshikamano kati ya viongozi na wananchi, hatua inayochangia kuboresha afya na kukuza umoja wa kitaifa.

Sillo pia ameipongeza CRDB Bank  kwa kuendelea kudhamini bonanza hilo kwa miaka kadhaa, akisema mchango wake umewezesha tukio hilo kukua na kuvutia ushiriki mkubwa zaidi kila mwaka.

Pamoja na hayo amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya Bunge, taasisi mbalimbali na wadau wa maendeleo katika kuendeleza sekta za michezo, ustawi wa jamii na maendeleo ya Taifa kwa ujumla.