Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online-Dar
MGOMBEA Ubunge Jimbo la Ukonga wilayani Ilala mkoani Dar-es-Salaam kupitia Chama Cha Mapindizi(CCM),Jery Silaa,ameeleza namna utekelezaji wa ilani ya chama hicho utakavyolibadirisha jimbo hilo na kuwa la kisasa .
Silaa amesema hayo katika uzinduzi wa kampeni za jimbo la Ukonga,ambapo wagombea udiwani saba wa jimbo hilo walitumia nafasi hiyo kujinadi kwa wananchi ili wawapigie kura ifikapo Oktoba 29 mwaka huu katika uchaguzi mkuu.

Amesema katika kipindi kilichopita amefanikiwa kusimamia utekelezaji wa ilani ya CCM hkatika sekta mbalimbali ikiwemo ujenzi wa tenki la maji Kata ya Pugu Bangulo linalohudunia eneo hilo,Gongolamboto,Kitunda mpaka jimbo la Kivule.
Pia ujenzi wa hospitali ya mama na mtoto ya nguvu kazi Chanika,kituo cha afya Zingiziwa,Buyuni,Mvuti,Pugu Station ,Mzinga Kituo cha afya Ghorofa mbili, Gongolamboto na jengo la macho katika Hospitali ya Wilaya Kivule.
katika sekta ya elimu shule za kisasa zimejengwa ikiwemo ya Nyeburu,Kigezi chini,Yongwe,na shule za Sekondari Ukonga ya ghorofa mbili,Nguvu mpya,Zogoali,Gulukwa Kwalala huku sekta ya miundombinu barabara zimejengwa ikiwemo ya njia sita mwendokasi Gongolamboto-Kariakoo mpaka Posta huku nishati ya umeme inapatikana kwa asilimia 100 kwa wananchi wote.
Amesema akipata ridhaa tena ya kuwa Mbunge wa Jimbo hilo,hata hakikisha Ukonga inakuwa ya kisasa ambalo masoko ya kisasa yatajengwa Gongolamboto ,Zingiziwa,Chanika ili wajasiriamali waweze kukuza uchumi wa nchi yao.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi(CCM), Wilaya ya Ilala,Said Sidde,amesema mpaka sasa chama hicho kwa Wilaya kina kata nane ambazo wagombea wake wamepita bila kupingwa wanasubiri kupigiwa kura za ndio au hapana.


More Stories
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI