Na Judith Ferdinand, TimesMajira Online, Mwanza
Siku 365 za Rais Samia Suluhu Hassan madarakani na mafanikio ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani Nyamagana mkoani Mwanza ikiwemo ya sekta ya elimu,afya,maji na ardhi.
Ambapo ndani ya kipindi hicho cha siku 365 Wilaya ya Nyamagana imepokea mabilioni ya fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika sekta mbalimbali,chini ya uongozi wa Rais Samia tangu kuingia madarakani baada ya mtangulizi wake Rais wa awamu ya tano Hayati Dkt.John Magufuri kufariki Machi 17,2021.
Akiwasilisha ripoti ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi pamoja na taarifa ya mafanikio hayo katika hafla ya siku 365 za Rais Samia Wilaya ya Nyamagana, Mkuu wa Wilaya hiyo Amina Makilagi, amesema Serikali ya awamu ya sita imedhamiria kuleta maendeleo kwa kujenga uchumi wa viwanda ili kuchochea uchumi ifikapo
2025.
Makilagi ameeleza kuwa katika kipindi hicho Rais amefanikiwa kutekeleza miradi ya kimaendeleo katika sekta mbalimbali wilayani humo ikiwemo,elimu,afya,maji,barabara,kilimo, kuwezesha makundi maalumu na sekta nyingine za kiuchumi,lengo ikiwa ni kuendelea kuleta maendeleo yenye tija kwa wananchi.
Sekta ya elimu
Makilagi amesema katika kuboresha,kuimarisha elimu na kujenga taifa la watu walioelimika serikali chini ya Rais Samia imejenga jumla ya vyumba 103 vya madarasa ambapo kati ya madasara hayo 64 yamejengwa kwa mfumo wa ghorofa na 36 yasiyo ya ghorofa,kwa fedha za Uviko-19 zaidi ya bilioni 6 huku Halmashauri ya Jiji ikichangia bilioni 1.9 za mapato ya ndani kwa upande wa sekondari.
Ameeleza serikali ilitoa kiasi cha milioni 470 kati ya milioni 600 za ujenzi wa shule mpya ya sekondari katika Kata ya Mkolani ambayo ujenzi wake unaendelea yenye madarasa 8,maabara 3,ofisi 2,jengo la utawala, maktaba,ICT, matundu 20 ya vyoo na nyumba ya walimu.
Pia ameeleza kuwa wanaendelea na ukamilishaji wa vyumba vya madarasa na ofisi za walimu katika shule za sekondari Bulale,Sahwa na Lwanhima,ukarabati wa madarasa 3,maabara na vyoo matundu 8 katika shule ya Sekondari Nyakurunduma,ukarabati wa shule ya msingi Nyanza English Medium,ukamilishaji wa bweni la wanafunzi wa mahitaji maalum katika shule ya msingi Buhongwa.
Akielezea suala la wanafunzi waliojiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka 2022, amesema idadi imeongezeka kutoka asilimia 80 mwaka 2021 hadi kufikia asilimia 84 mwaka huu,ambapo walilenga kusajili wanafunzi 10,007 kati ya wanafunzi 11,884 waliochaguliwa.
Pia ameeleza kuwa,katika kipindi cha mwaka 2021 sekta ya elimu ilikuwa na mafanikio chanya ambapo ufaulu kwa wanafunzi wa darasa la nne ulikuwa asilimia 98 kati ya lengo la asilimia 100 na kushika nafasi ya kwanza kimkoa,darasa la saba asilimia 97.4 na kushika nafasi ya kwanza,kidato cha nne, ufaulu ulikuwa asilimia 93.9 huku kidato cha sita ukiwa ni asilimia 97.
Aidha ameeleza kuwa uandikishaji wa wanafunzi wa darasa la kwanza umeongezeka kutoka asilimia 95 mwaka 2021 hadi asilimia 100 mwaka 2022,ambapo matokeo ya uandikishaji kwa darasa la kwanza mwaka huu lengo ilikuwa wanafunzi 14,573 ambapo uandikishaji halisi ulikuwa wanafunzi 15,509 sawa na asilimia 106.
Huku uandikishaji kwa dasara la awali lengo ni 7,201 ambapo uandikishaji halisi ulikuwa 6,708 sawa na asilimia 93 na uandikishaji bado unaendelea.
Sekta ya Afya
Makilagi ameeleza kuwa katika sekta ya afya,imeendelea kuboreshwa,ambapo hospitali ya Rufaa ya Sekou-Toure,imesimika mashine ya CT Scan yenye thamani ya bilioni 2, jengo la mama na mtoto limekamilika kwa asilimia 98 ambapo kiasi cha biilioni 9.8 kati ya bilioni 10 zimetumika,milioni 665.1.zimetumika kununua dawa na vifaa tiba,pia wilaya ilipokea milioni 167 kutoka Mfuko wa Pamoja.
Aidha mashine mpya ya mionzi (X-ray) yenye thamani ya milioni 280 imefungwa hospitali ya Wilaya ya Nyamagana,mashine ya utambuzi wa magonjwa kwenye damu (full blood picture machine) imenunuliwa kwa kiasi cha milioni 8 huku mashine 4 za kusafisha figo zikifungwa hospitali Sekou-Toure.
Pia amesema Wilaya ilipokea kiasi cha milioni 59 ambazo zimetumika katika uhamasishaji na uchanjaji wa chanjo ya Uviko-19 ambapo hadi sasa jumla ya wananchi 33,398 wameisha pata chanjo na zoezi linaendelea.
Sekta ya Maji
Makilagi amesema wilaya hiyo ilipokea bilioni 140.3 kwa ajili ya kuboresha huduma za maji ambapo mradi wa ujenzi wa chanzo kipya cha maji cha Butimba unagharimu kiasi cha bilioni 69.3 na utawanufaisha wananchi 300,000 wa pembezoni mwa Jiji pamoja na miradi ya miundombinu ya maji ikiwemo tenki la maji Mahina na Sahwa.
Sekta ya Ardhi
Makilagi ameeleza kuwa katika kipindi hiki cha mwaka mmoja wa Rais Samia madarakani,upande wa ardhi na makazi, asilimia 75 ya migogoro imetatuliwa na kupelekea makusanyo ya kiasi cha zaidi ya bilioni 3, vipande 79,937 vya ardhi vimetambuliwa,viwanja 52,333, vimepimwa na viwanja 17,577 vimemilikishwa.
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi