Na Heri Shaaban, Timesmajira Online,Ilala
SHULE ya sekondari Kisutu ya Wasichana iliopo wilayani Ilala, wajivunia mafanikio ya kitaaluma kwa miaka mitatu mfululizo kutokana na ufaulu wa kidato cha sita kupanda mwaka hadi mwaka.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa shule hiyo Chiku Mhando katika mahafali ya saba ya kidato cha sita ambapo wahitimu 318 walitunukiwa vyeti.

Ambapo amesema mwaka 2022 jumla ya watahiniwa 262 walifanya mtihani wa kidato cha sita,kati yao 40 walipata daraja la kwanza, 135 walipata daraja la pili, 84 walipata daraja la tatu na watatu walipata daraja la nne.
Mwaka 2023, watahiniwa walikuwa 249,kati yao 68 walipata daraja la kwanza, 134 walipata daraja la pili,47 walipata daraja la tatu.Huku mwaka 2024 kulikuwa na jumla ya watahiniwa 293,kati yao 94 walipata daraja la kwanza,144 walipata daraja la pili, 54 walipata daraja la tatu na mmoja alipata daraja la nne.
Amesema,mikakati na matarajio ya walimu na uongozi wa shule katika mtihani wa kidato cha sita utakaofanyika Mei mwaka huu,hakutakuwa na mwanafunzi atakayepata daraja la nne wala daraja sifuri badala yake wanafunzi wengi watapata daraja la kwanza na la pili huku wanafunzi wachache watakaopata daraja la tatu.

Pia amesema,kwa sasa shule ina jumla ya wanafunzi 679,kati yao wa kidato cha sita ni 318 na kidato cha tano ni 361 huku masomo wanayofundishwa ni mchepuo wa PCM, PCB, CBG, HGL, HGK na HKL.

More Stories
Rais Mwinyi aipongeza Kampuni ya Yas kushirikiana na ZHC
Raha ya WiFi za bure na mtego kwa taarifa zako za siri
Mke wa Rais wa Finland atembelea Makumbusho ya Taifa