November 22, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Shule maalum za bweni na maono ya Rais Samia kuzalisha wanasayansi ya wanawake

Na Jackline Martin,TimesmajiraOnline,Dar

RAIS Samia Suluhu Hassan, aliposema Serikali yake inaanza ujenzi wa Shule Maalum za Bweni kwa ajili ya wasichana, wapo waliodhani uamuzi huo utachukua muda mrefu kutekelezeka.

Wapo waliodhani hivyo, kwani kukamilika kwa mpango huo pengine kunaifanya Tanzania kuwa nchi ya kwanza Afrika kuwa na shule za aina hiyo, zimejengwa 26, kila mkoa shule moja kwa gharama za sh. bilioni.

Katika kufanikisha mpango huo, Serikali ya Samia, ilitoa fedha za za kujenga shule mpya maalum za Sekondari za Bweni kwa ajili ya wanafunzi wa kike katika mikoa yote nchini.

Kupitia mradi wa kuboresha Elimu ya Sekondari (SEQUIP) wa miaka mitano, Serikali ilitenga sh. Trilioni 1.2 kwa ajili ya kujenga shule mpya za Sekondari 1,026 kati ya hizo, shule 26 ni shule Maalum za wasichana 26, kila mkoa shule moja.

Kupitia mradi wa kuboresha Elimu ya Sekondari kila mkoa umepewa bilioni 4 kwa awamu mbili kujenga shule ya wasichana ya bweni, ambayo itakuwa na uwezo wa kupokea wanafunzi 1,080 na kidato cha kwanza hadi cha sita.

Katika mwaka wa fedha wa 2021/2022 Serikali ilipeleka sh. bilioni 30 kwenye mikoa 10 ambapo kila mkoa ulipokea Bilioni 3 za awamu ya kwanza kwa ajili ya kujenga shule za Sekondari za wasichana.

Aidha, Dkt. Msonde amesema Katika mwaka wa fedha 2022/23, Serikali tayari Serikali imepeleka fedha katika mikoa 16 iliyosalia, ambapo mikoa yote 26 nchini inaendelea na utekelezaji wa shule hizo ambazo zimekamilika na kuanza kupokea wanafunzi.

Kinyume na matarajio ya wengi, tayari shule hizo zimeanza kupokea wanafunzi dhamira ikiwa ni kuongeza idadi ya wanafunzi wa kike wa fani za sayansi

Ujenzi wa shule hizi za bweni za Sayansi kwa wasichana ni mkakati maalum wa Serikali ya Rais Samia kuhakikisha anawasogeza karibu wanawake na ukuaji wa kasi ya teknolojia pamoja na kuendana na mahitaji ya sasa ya Dunia.

Aidha, hatua hiyo itaongeza fursa kwa wanafunzi wa kike kupata nafasi zaidi za kujiunga na masomo ya michepuo ya sayansi katika vyuo vikuu mbalimbali nchini.

Hadi sasa sehemu kubwa ya shule hizo 26 wasichana za masomo ya Sayansi 26 nchini zimeanza kutoa hamasa zaidi kwa kuongeza udahili wa wanafunzi wanaosoma sayansi.

Shule hizo zitakuwa mwarobaini wa kupunguza tofauti kubwa iliyopo baina ya wanaume na wanawake wanaodailiwa kwenda vyuo vikuu kwa upande wa masomo ya sayansi.

Hatua hiyo itashawishi wasichana kusoma masomo hayo, hivyo kuleta uwiano sawa baina ya wanawake na wanaume.

John James (49) anapongeza Serikali ni kuongeza udahili kwa kujenga shule za wasichana za masomo ya sayansi nchini

”Nimepokea uamuzi wa Serikali kwa mikono miwili, kwani utahamasisha kozi za sayansi zinazotolewa katika vyuo vikuu nchini pamoja na kutekeleza mkakati wa kujenga shule za masomo ya Sayansi 26, huku kila mkoa ikijengwa moja,” alisema na kuongeza;.

“Ujenzi huu wa Serikali huenda Tanzania ikawa ndiyo nchi ya kwanza Afrika Mashariki kujenga shule maalum za wasichana ili wasome masomo ya Sayansi tu.”

Anasema ni wazi kwamba Rais Samia ametambua wasichana wengi hawawezi kufikia uwezo wao kikamilifu kwenye shule ya mchanganyiko.

“Kwenye shule za mchanganyiko wasichana wengi wanaathiriwa zaidi na suala la rika na taama, Hizi ni baadhi tu ya sababu ambazo hufanya wasichana wengi kuzuia ubinafsi wao katika mazingira ya kitaaluma,” alisema.

Mwalimu Mstaafu, Shaban Abdallah, anasema wasichana wanapokuwa wanasoma kwenye shule za jinsia moja wanakuwa na ujasiri wa kupuuza ubaguzi wa kijinsia na kuendeleza ushindani wao kikamilifu katika mazingira ya kitaaluma ya jinsia moja.

“Panakuwa hakuna wavulana wa kuwashangaza, hakuna wavulana kushindana kati ya wasichana wengine. Hawana haja ya kuwa na wasiwasi juu yao kila mmoja anajisikia kuwa mwenyeji,” anasema.

Anasema Rais Samia anajua fika kwamba kuwaanda wanafunzi wa kike kwenye masomo ya sayansi ni kuwaanda kufanyakazi ambazo huko nyuma ziliuwa zikitazamwa kama kasi za wavulana peke yake.

Aidha, anasema uamuzi huo wa Rais Samia unalenga pia kuwaanda wanawake kuwa viongozi .

anasisitiza kwamba wanafunzi wasichana wanahisi huru zaidi wa kuzungumza na kujieleza wenyewe, hatu ambayo inasababisha maendeleo ya nguvu ya upendo wa kujifunza. Shule za wasichana zinaweza kutoa fursa zaidi za kufanikiwa

Tafiti zinaonesha kuwa zaidi ya asilimia 80 ya wahitimu kutoka shule zote za wasichana wanasema kwamba wanazingatia utendaji wao wa kitaaluma kama mafanikio makubwa .

Wanafunzi waliosoma shule za jinsia moja wanaripotiwa kuwa na ujasiri zaidi kuliko wenzao katika shule za mchanganyiko.

Mmoja wa wanafunzi aliyesoma shule ya wasichana Rugambwa, mkoani Kagera, Joyce Damian, anasema shule za wasichana zisaidia binti awe vyovyote anayotaka.

“Licha ya uhaba wa wanafunzi wa kike kusoma masomo ya sayansi nchini, bado kuna changamoto mbalimbali zinazowakabili baada ya kuhitimu masomo hayo.”

Afisa Mpango Ujenzi wa Nguvu za pamoja na harakati kutoka Mtandao wa Jinsia Tanzania, Flora Ndaba, anasema kuwa moja ya jukumu kubwa wanalolifanya kwa sasa ni kueneza uwazi kwa wasichana kutambuwa umuhimu wa masomo hayo licha ya wanafunzi wengi kuacha kuchagua masomo ya sayansi wafikapo shule za upili.

Aidha, anasema kumekuwa na mwamko mdogo kwa wanafunzi wa kike kusomea ufundi na pindi wanapohitimu masomo hayo hujishughulisha na biashara mbadala badala ya kutumia taaluma zao.

Mwalimu Paul Ezekiel pamoja na wanafunzi waliosomea fani mbalimbali katika Chuo Cha Ufundi VETA Dodoma, wanasema changamoto kuu ni ushawishi katika kazi pamoja na wengine kuacha kutumia taaluma zao baada ya kuingia katika maisha ya ndoa.

Sanjari na hayo Mwalimu Ezekiel amewashauri wanafunzi wa kike kujituma katika taalumu za ufundi wanazosomea ili kujikomboa katika wimbi la ukosefu wa ajira.