November 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Shule iliyoongoza kitaifa  kwa kuwa ya kwanza katika matokeo ya mtihani wa Taifa wa darasa  nne yatoa siri ya mafanikio

Na Esther Macha,Timesmajira,Online, Chunya

UONGOZI wa shule ya awali na msingi ambayo ni mchepuo wa kiingereza  ya Holy land iliyopo katika mji wa Makongorosi Wilayani Chunya umesema kuwa shule hiyo ina malengo endelevu ambayo hayawezi kukomea kwenye sifa ya kushika nafasi ya kwanza kitaifa katika matokea ya mtihani wa wa Taifa wa darasa la nne mwaka 2021 kwa shule zenye wanafunzi chini ya 40.

Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa shule ya Holyland Pre &Primary School , Yona Mwakalinga wakati akizungumza na Times majira ofisini kwake jana kuhusiana na shule hiyo kushika nafasi ya kwanza kitaifa,kimkoa na kiwilaya licha ya kuwa changa toka kuanzishwa kwake .

“Sisi unajua katika shule yetu hii ni mara yake ya  kwanza  kufanya mtihani wa taifa wa darasa la nne  na mtihani wa majaribio tuliongoza  na hatukulizika  tukliendelea kufanya juhudi  na kujituma zaidi na haya ndo matokeo yake kuongoza mtihani wa Taifa lakini sisi tunachukulia kama ni changamoto  hatuwezi kufurahia na kujisahau na kulewa sifa hizi bali tunaendelea kupigana kadri ya uwezo wetu ili tuendelee kubaki kwenye nafasi yetu ,kwa hiyo sisi tumechukua hili kama sehemu ya changamoto kwetu ambayo itatufanya tuendelee kujituma zaidi  ya hapa kwasababu kushika nafasi ya kwanza kitaifa sio jambo dogo kwa hiyo asilimia  kubwa wananchi wanaangalia shule hiyo mitihani inayokuja  inafanya nini”amesema Mwalimu Mwakalinga.

Hata hivyo Mkuu huyo wa shule amesema kwamba akiwa kiongozi wa shule hiyo atahakikisha anakuwa na usimamizi mzuri na ushauri kwa  wafanyakazi na walimu na ikiwezeka na zaidi ya pale ili kuweza kuilinda nafasi hiyo  na kwamba lengo la shule hiyo kutoa elimu bora kwa watoto na kwamba elimu bora inathibitishwa kupitia mitihani .

Aidha Mwakalinga amesema kuwa  wanahitaji mchango mkubwa kutoka kwa wadau ili kuweza kuboresha maeneo ambayo hayajakaa sawa  kwasababu lengo ni kufikia malengo mazuri zaidi ili kuweza kutoa elimu vbora ikiwa ni pamoja na nidhamu kwa watoto na elimu bora.

Akielezea zaidi mahusiano ya walimu na wafanyakazi wa shule hiyo kwa watoto Mkuu huyo wa shule amesema ni pamoja na ukaribu  kwa watoto, miundo mbinu ya shule ambayo ni michezo ,sinema za picha za wanyama hivyo kuwafanya watoto kupenda shule  kutojisikia ukiwa kutokana na kuwa mbali na wazazi wao hivyo watoto kuona wapo sehemu sahihi kwao.

Kwa upande wake Mwalimu wa Taaluma katika shule ya HolyLand , Ally Nashon amesema kwamba sifa ya kwanza iliyopelekea shule hiyo kushika nafasi ya kwanza kitaifa kwenye kundi lao kimkoa na wilaya ni mkurugenzi wa shule hiyo Lawena Nsonda (Baba mzazi) kuwa bega kwa bega na walimu na kutoa vifaa vya kufundishia kwa wakati  na mahitaji mengine muhimu kwa wafanyakazi  kutoa motisha kwa walimu wanaofanya vizuri,kufanya kazi kwa ushirikiano na walimu na wafanyakazi na kwamba kila mtu anacheza kwa nafasi yake kwa umakini .

“Lakini pia watoto wetu wana nidhamu kubwa kama unavyojua taaluma bila nidhamu haiwezekani ,imefika hatua motto wa darasa la nne  na tano huwezi kukuta mtoto anapiga kelele zaidi muda mwingi anakuwa  bize kujisomea  vitu ambavyo vinapelekea mtoto kuwa na uelewa mzuri wa kimasomo ambao unatokana na juhudi za walimu za kuhakikisha kuwa mtoto anakuwa  katika maadili mema na kuwa ari ya kupenda elimu “amesema Mwalimu Nashon.

Akizungumzia kuhusu idadi ya wanafunzi waliofanya mtihani wa Taifa wa darasa la nne mwaka 2021 kwa shule hiyo Mwalimu Nashon amesema kwamba walikuwa na watoto saba (7) kati yao wa kiume watatu na wa kike wanne ,na kwamba hivi sasa shule imeingia kwenye vita na kuuliza shul;e hiyo haimna muda mrefu kwanini ishike nafasi ya kwanza kitaifa hivyo ni lazima kujipanga  na pia mkurugenzi wa shule ameongeza motisha kwa walimu na wafanyakazi shuleni hapo ili waweze kuwa moyo wa kufundisha na kuhudumia watoto.

Kwa upande wake Diwani wa viti wa maalum kata ya Makongorosi Wilayani Chunya , Sophia Mwanautwa amesema kuwa Wilaya hiyo miaka ya nyuma ilikuwa nyuma kielimu lakini imeendelea kuwa vizuri na mpaka matokeo ya mtihani wa Taifa imeshika nafasi ya kwanza kitaifa na kimkoa kuongoza pamoja na kiwilaya.

“Mmiliki wa shule hii amekuwa mkombozi kwa wilaya yetu binafsi nina watoto wangu wawili wanasoma Holyland  sijutii wanangu wapo vizuri kielimu  nawaomba wazazi tuliopo katika Mji wa Makongorosi tupende elimu  maana ndo mkombozi kwa watoto wetu ,tunamshukuru Rais wetu mama Samia Suluhu Hassan kutupatia madawati na  vyumba vya madarasa vya kutosha watoto wote wanaenda shule labda iwe uzembe kwa mzazi au mlezi”alisema Mwanautwa.

Mkuu wa shule ya Holyland Yona Mwakalinga akizungumza na mtandao huu

Mwalimu wa Taaluma Ally Nashon akifafanua jambo