Na Penina Malundo,Dar es Salaam
FAMILIA ya Said Nkya kwa kushirikiana na Chama cha Gofu cha Wanawake Tanzania (TLGU), wameandaa shindano linaloitwa Lina PG Tour kwa ajili ya kumuenzi mchezaji wa gofu wa zamani anayeitwa Lina Nkya.
Shindano hilo litakalofanyika mwaka mzima katika viwanja mbalimbali vya Golf ikiwemo mkoa wa Dar es Salaam, Kilimanjaro Arusha na Zanzibar.
Wakizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana familia hiyo na TLGU walisema zaidi ya wachezaji wa kulipwa, ridhaa, vijana na watoto 100 watashiriki mashindano hayo na washindi kushinda zawadi za fedha zitakazovunja rekodi.
“Lina alikuwa mchezaji gofu makini hapa Tanzania hivyo katika kumuenzi tunataka tuendelee kuibua wengi watakaopeperusha bendera ya taifa, Mungu amlaze mahali pema peponi,”amesema Makamu wa Rais wa TLGU Ayne Magombe.
Kwa upande wake, kiongozi wa familia hiyo Said Nkya (mume wa Lina) amesema mke wake alikuwa akiupenda sana mchezo huo kiasi cha kuibua wachezaji wengi wa kulipwa kupitia klabu ya Moshi jambo ambalo wameona waliendeleze kuibua wachhezaji wengine ambao wapo chini.
Amesema wameandaa zawadi nzuri kutoa motisha kwa vijana wadogo kuongeza bidii na kuonesha kiwango cha juu ili kutamani kuwafikia waliofanya vizuri.
Amesema mashindano hayo yanalengo la kuwainua vijana katika kucheza michezo hiyo na ili waweze kuipenda wataweza kutoa zawadi nzuri ili kuhamasisha wachhezaji.
“LINA PG ni mashindano yanayoenda kuhamasisha wachezaji wachini kuja juu, wa katikati kupata na wale wabobezi (Professional) kwenda juu zaidi la kuwa kundi la Senior,”amesema na kuongeza
“Vijana hao wanaochipukia tunawaandaa kwa muda wa Mwaka mmoja hadi miwili kuwavuta kutoka walipo chini hadi kuwaaandaa kwa kipindi hicho na kuja kuwa wachezaji wazuri nchini,”amesema
Kwa Upande wake Katibu wa Mashindano wa TLGU, Rehema Athumani amesema mashindano hayo yatafanyika kuanzia Februari 29 hadi Machi 3 katika klabu ya TPC iliyopo Moshi.
Amesema yatafanyika pia, Zanzibar April 11 hadi 14, Arusha Gymkhana Julai 11 hadi 14, Klabu ya Moshi na Dar es Salaam itakuwa Novemba 14 hadi 17 klabu ya Gymkhana na yatakuwa endelevu kila mwaka
More Stories
Jokate awapa tano vijana UVCCM maandalizi Mkutano Mkuu wa CCM
Watakaokwamisha mapato Kaliua kukiona cha moto
Dkt.Gwajima aagiza kuundwa kamati za ulinzi wa watoto