Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online
MSANII wa muziki wa Bongo fleva na Mjasiriamali hapa nchini Zuwena Mohamed maarufu kama ‘Shilole’, Ijumaa hii anatarajia kufungua Mgahawa wake rasmi ujulikanao Shishifood katika Jiji la Dodoma kwa ajili ya kuwahudumia wakazi wa mji huo wakiwemo Wabunge wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akiweka wazi hilo kumpitia kwenye Ukurasa wake wa Instagram Shilole amesema, alikuwa na doto kwa muda mrefu kuwa siku moja aweze kufungua Mgahawa katika Jiji la Dodoma jambo ndoto zake zimetimia.
“Ilianza kama ndoto tu niliyoiota kwa ajili ya ndugu zangu wa Dodoma. Nikawaza kwanini zile ladha za chakula cha kitazania ziishie Dar tu?. Nikajiuliza kwanini na watu wa Dodoma nao wasile kujigalagaza?, Kwa mfano msimu huu bunge likiwa linaendelea kwanini wabunge nao wasifaidi chakula chetu cha asili chenye ladha ya kiafrika?.
“Waheshimiwa wabunge wengi sana hupenda chakula chetu cha Shishifood. Sasa ni rasmi kila mtu alieko Dodoma anayo ruhusa ya kula kujigalaza. Leo nimepita pale mjengoni kuwapelekea salamu zangu Ijumaa hii tunaifungua rasmi Shishifood in Dodoma,” amesema Shilole.
More Stories
Startimes yazindua makala ya China, Africa
Mwanasheria wa Katavi aliyetimkia kwenye muziki achaguliwa tuzo za MIEMMA
Coca-cola ‘Kitaa Food Fest’ yahitimishwa kwa mafanikio