December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Shilole amuomba Dc Jokate kuwaongezea muda wa kufanya biashara Sabasaba

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online

MSANII wa muziki wa Bongo fleva na Mjasiriamali hapa

nchini Zuwena Mohamed maarufu kama ‘Shilole’, kwa

niaba ya wasanii wenzake amemuomba Mkuu wa Wilaya ya

Temeke Jokate Mwegelo kwaongezea muda wa kufanya

biashara katika viwanja vya Sabasaba, Dar es Salaam.

Akitoa ombi hilo, katika uzinduzi wa ‘Meet Your Star’

jana Shilole amesema, kwa sasa muda wa kufanya

biashara katika mabanda yao ya wasanii ni saa ne hivyo

wanahita waendelee hadi saa sita kwa ajili ya kuwapa

nafasi ya kutosha mashabiki zao.

Mbali na hivyo Shilole amesema, wanaomba ulinzi wa

kutosha katika mabonda yao ya wasanii, barabara kuwa

nyeupe na hawaitaji umeme ukatike pamoja na maji ya

kutosha, ili waweze kufanya biashara zao kwa umakini

mkubwa.

Amempongeza muandaaji wa ‘Meet your Star’

ZamaradiMkekema kwa kuandaa kitu hicho kwani kimewapa

fursa wasanii kuuza bidhaa zao ili waweze kujikwamua

kiuchumi.