December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Shilole afunga ndoa rasmi na Rommy

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira online

MSANII wa muziki na Mjasiriamali hapa nchini Zuwena Mohamed maarufu kama ‘Shilole’, ameweka wazi kuwa amefunga ndoa na aliyekuwa mchumba wake wa hivi karibuni Rajab Issa maarufu ‘Rommy’ kwa ajili ya kumpendeza mwenyezi Mungu.

Akiweka wazi hilo, Kupitia kwenye ukurasa wake wa Instagram jana, Shilole ameshukuru mara baada ya kufunga ndoa na kusema wamemaliza salama ambapo kwa sasa anaitwa Mrs Rommy.

“Alhamdulillah tumemaliza salama, rasmi ni mume na mke niliechukuliwa kwa furaha na upendo wa juu ‘Officially Husband and Wife happily taken and very much in love’ kwasasa unaweza kuniita Mrs Rajab Issa (Rommy) Yarabbi iwe salama,” ameandika Shilole.

Kabla ya hapo Shilole alikuwa kwenye ndoa na mfanyabiashara Uchebe na waliachana mwaka jana baada ya ugomvi mkubwa uliotokea kwenye ndoa yao.