February 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Shigongo: Rais Samia ameleta mafanikio mengi katika kukuza uchumi

Na Mwandishi wetu Timesmajira online

MBUNGE wa Jimbo la Buchosa, Erick Shigongo amesema katika kipindi kifupi cha uongozi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amefanya mafaniko mengi hususani katika kukuza uchumi wa nchi na mtu mmoja

Shigongo ameyamebainisha hayo Jijini Dar es salaam mapema leo Februari 22,2025 wakati akizugumza na waandishi wa habari kuhusu masuala mbalimbali ya kisiasa hususani katika Jimbo lake.

Amesema kutokana na mafanikio hayo watanzania wanapaswa kutumia utajiri uliopo nchini kwa kuleta maendeleo huku wakimsaidia Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kukuza uchumi huo.

“Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu imefanya mambo mengi ya kimaendeleo katika Jimbo la Buchosa pamoja na kukuza uchumi wa nchi na mtu mmoja”amesema

Amefafanua kuwa ndani ya miaka mitatu kwa upande wa Jimbo la Buchosa limepokea sh.bilioni 62.5 kwa shughuli za maendeleo ambazo zimejenga vituo vipya vya afya vitano, sekondari zaidi ya nane, zahanati 21 na madarasa kadhaa.

Aidha aliwataka Watanzania kujivuna kwa kuwa na uchumi unaofanya vizuri ndani ya uongozi wa Rais Dk.Samia ikilinganisha na nchi nyingine za jirani.

“Tanzania sasa ina bahati ya kuwa na uongozi bora kwa sababu Rais Dk.Samia ameamua kutumia utajiri wetu kuleta maendeleo kwa kupunguza utegemezi, hivyo Watanzania tumieni utajiri kuleta maendeleo”amesema

Kwa upande wa utalii amesema kupitia filamu alizocheza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imeleta mapato makubwa takribani dola za kimarekani bilioni sita, na kufanya uwekezaji katika kilimo hususani cha umwagiliaji lengo likiwa kumwinua Mtanzania na kumuondoa katika umaskini