December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Shibuda ampongeza Makonda

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Vyama Vya Siasa, MNEC Mstaafu na Mbunge wa (CCM 2005 na CHADEMA 2010) Magalle Shibuda ampongeza Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Paul Makonda kwa juhudi na shabaha za kuunda daraja rafiki kazi za Rais Samia na Watanzania.

Asema Makonda amejenga uhusiano rafiki wa Kanda ya Ziwa kwa kutoa ahsante kwa uwajibikaji wa serikali.

Amejenga na kuleta wokovu wa mlango wa kutokea huzuni za ndani zilizounda ugumu wa mioyo katika kufumbua maono ya ahsante

Shibuda ametoa barua aliyoandika Manufaa na Faida kwa Chama Cha Mapinduzi kutokana na ziara ya Mikoa ya Kanda ya Ziwa iliyofanywa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Paul Makonda.

Katika barua hiyo,Shibuda ameandika kuwa ziara ya Mwenezi Makonda imebainisha wazi kuwa kuna maisha ya wajibu wa uzalendo hitajika wa kufaidisha manufaa ya maslahi mapana kwa ujenzi wa kuunda ustawi na maendeleo ya jamii, uchumi na Taifa.

Shibuda amesema Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan anastahili tuzo za utu kwa hali na sababu ni kiongozi mkwamuaji wa madhila yaundayo huzuni.

Amesema kwa kuthibitishi hilo, Watanzania warejee kwa uundwaji wa kamati kadhalika mfano ya Jaji Mstaafu Othman Chande ya kuimairsha haki za raia.

Ameendelea kuandika kuwa ziara ya Mwenezi Makonda imewadhiirishia umma kuwa serikali ya awamu ya 6 ina unyenyekevu wa kutumikia maslahi ya umma na kusema kuwa simu zote kwa Mawaziri ni fursa rafiki kwa umma nao utambue kwa umakini na ukubali kuwa ni uwazi na ukweli pana mipango ya kazi za kutengua kasoro zinazounda sintofahamu kwa yao matumaini na matarajio ya Wananchi.

Pia Shibuda amesema binafsi yake ameona Mwenezi Makonda ameunda vema somo la kwamba Serikali ina wajibu wa kukithaminisha chama kinachoongoza Serikali hiyo ambacho ni CCM.

Vivyo hivyo CCM ina wajibu wa kuisadikisha tija ya Serikali yake ndani ya umma dhidi ya propaganda hasi za vyama kinzani.

Aidha amemtaka Mwenezi Makonda kuendelea kusomesha kuhusu yeye anatenda uwajibikaji wake aminifu kwa Katiba ya Chama Cha Mapinduzi.

Kwa kumalizia Shibuda ametoa rai kwa CCM kuwa macho na kupambanua akili zao dhidi ya mikakati ya wazuaji wa tafsiri ovu ambazo zinataka kuunda hali ya kuchafuana wenyewe kwa wenyewe na kuwataka kutokuwa malighafi au kitoweo cha propaganda hasi za kujenga kuandika uongo mtamu dhidi ya umoja na mshikamano wao.