December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Shamsa: Tuache kuwaonga
wanaume, tunawapumbaza

Na Mwandishi Wetu

Msanii wa filamu za Bongo na Mjasiriamali hapa nchini, Shamsa Ford ametoa ujumbe mzito kwa wanawake wanaopenda kuwaonga wanaume.

Akitoa ujumbe huo kupitia kwenye ukurasa wake instagram, Shamsa amesema siku zote mwanaume ukimuonga pesa jua kuna sehemu anapeleka.

“Kuna kusaidiana kwenye mapenzi na kuhonga. Hapa nazungumzia wanawake wanaowahonga wanaume pesa ili wapendwe.

“Mfundishe mwanaume wako jinsi ya kutafuta pesa na si kumuhonga. Mwanaume unayemuhonga pesa kuna sehemu na yeye anapeleka ili aonekane kidume,” amesema Shamsa.