January 23, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Shamsa Ford: Tuishi na watu vizuri

Na Mwandishi Wetu

Muigizaji wa filamu za Bongo na Mjasiriamali hapa nchini, Shamsa Ford ameitaka jamii kuishi na watu vizuri huku akisema duniani ni mapito tu.

Akitoa ujumbe huo kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram, Shamsa amesema binadamu hana haja ya kulinga maisha ya duniani.

“Ishi na watu vizuri ipo siku utashindwa kufanya chochote na kusindikizwa kwenda nyumba yako milele kwa kubebwa.

“Huna haja ya kuringa haya maisha ya duniani tunapita tu. Usijione wewe ni muhimu sana kuliko wengine,” amesema Shamsa.