Na Mwandishi Wetu,TimesMajira Online,Singida
SERIKALI imewataka wafungwa nchini, kuzidisha kufanya ibada sambamba na kuzidisha kumuomba Mungu ili wakitoka waende kuwa raia wema pamoja na kukamilisha ndoto zao.
Kauli hiyo ilitolewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Khamis Chilo katika kikao cha ndani kilichohusisha wafungwa na mahabusu katika Gereza la Wilaya ya Sindida mjini.
Waziri huyo pia alipata fursa ya kuwasikiliza wafungwa ambao walitoa maoni, mapendekezo na changamoto mbalimbali walizokua nazo ikiwemo kuchelewa kwa upepelezi wa kesi zao.
“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, anawategemea sana hasa vijana na taifa hili linawategemea sana, hapa naona vijana mko wengi vijana ndiyo nguvu kazi ya taifa, sasa endeleeni kuwa raia wema, ukitoka hapa kifungoni nenda kawe raia mwema, mkitoka hapa nendeni mkaendeleze ndoto zenu.
“Fanyeni ibada muombeni Mungu sana, fanyeni ibada huwezi kujua ukitoka hapa utakwenda kuwa nani maana historia inatuonesha wako watu mbalimbali walikua wafungwa, lakini walivyomaliza vifungo vyao walikwenda kuwa viongozi wakubwa tu,” amesema.
Akisoma taarifa ya gereza mbele ya Naibu Waziri, Mkuu wa Gereza la Wilaya ya Singida, amesema katika gereza hilo kuna shughuli mbalimbali za uzalishaji ikiwemo kilimo cha mahindi, maharage, mbogamboga, ufyatuaji wa matofali, ufugaji wa samaki na ujenzi wa nyumba za makazi ya askari.
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba