December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

BREAKING: Serikali yatoa maelekezo ya ada kwa shule binafsi

Na Joyce Kasiki, TimesMajira Online, Dodoma

KUTOKANA na sintofahamu iliyojitokeza kwa baadhi ya shule binafsi nchini ya ulipaji ada, Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imeamua kuingilia kati suala hilo na kutoa maelekezo ya ulipaji ada katika shule hizo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara hiyo kwa umma(Pichani kushoto), kamati na bodi za shule zifanye uchambuzi wa gharama inayopaswa kupungua kwa siku ambazo wanafunzi hawakuwepo shuleni.

Juni 29 mwaka huu wanafunzi wanatarajia kurejea shuleni baada ya likizo iliyoanza tangu Machi mwaka huu kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa corona.

Hata hivyo kumekuwemo sintofahamu ya ulipaji ada katika shule binafsi kutokana na baadhi ya wazazi kuwa walishalipa ada kabla ya kufunhwa shule lakini baada ya shule kufunguliwa bado wanadaiwa walipe tena.