Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma
WIZARA ya Fedha na Mipango imetiliana saini ya makubaliano na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kwa ajili ya ulipaji wa fedha kiasi cha shilingi trilioni 2.17 kwa mfuko huo ili kuuwezesha PSSSF kuboresha utendaji wao wa kulipa mafao kwa wastaafu.
Akizungumza katika hafla ya makubaliano hayo,Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Emmanuel Tutuba alisema,PSSSF imekuwa na deni ililolirithi baada ya iliyokuwa mifuko ya Hifadhi ya Jamii kuvunjwa na kubaki na mfuko mmoja wa watumishi wa umma na hivyo Serikali kuamua kulipa deni hilo.
“Sisi kama Wizara tumekuwa na majadiliano mara kadhaa na uliokuwa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) na sasa PSSSF juu ya kushughulikia suala la deni la ‘pre 1999,baada ya kufanya uchambuzi wa kina juu ya suala hilo na kwa maslahi mapana ya wanachama wa Mfuko,Serikali imeamua kulipa deni hilokwa kuanzia n ash.Trilioni 2.17 ,na deni hilo litalipwa kwa utaratibu wa hati fungani maalum ya kuanzia miaka nane hadi 25.”alisema Tutuba
Alisema,kutokana na makubaliano hayo ,anaamini ufanisi na utendaji wa Mfuko utaongezeka haswa katika kuwahudumia wanachama wa Mfuko huo ambao wengi sasa wamestaafu.
“Tangu iliyokuwa PSPF imekuwa ikiomba Serikali kuiongezea uwezo ili iweze kulipa kiinua mgongo na pensheni za mwezi kwa watumishi wa umma ambao walikuwepo katika ajira kabla ya mwaka 1999.”alisema Tutuba
Alisema,mpaka sasa Serikali imeshailipa PSSSF kiasi cha shilingi bilioni 500 kati ya shilingi bilioni 724 za deni lililohakikiwa na inaendelea kulipa deni hili lengo likiwa ni kuona Mfuko huo pamoja na sekya ua Hifgadhi ya Jmaii kunakuwa na Ustawi unaotakiwa na hatimaye kulinda amslahi ya wadau kwa muda mrefu ujao .
“Ni matumaini ya Wizara kuwa fedha hizi zitasaidia katika kulipa mafao kwa wakati ya wanachama wenu wanaostaafu ,kuendelea kulipa kwa wakati pensheni za mwezi kwa wastaafu wetu na pale zitakapotumika katika uwekezaji basi uwe wenye tija ambao utasaidia kukuza thamani ya Mfuko na hivyo kutiumiza wajibu wenu kwa muda mrefu ujao.”alisisitiza
Kwa mujibu wa Tutuba,nia ya Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ni kuona wastaafu ambao wamelitumia Taifa letu wanafurahia maisha yao ya ustaafu .
“Hivyo baada ya kusaini makubaliano yetu,ni matarajio yetu kuwa malalamiko kutoka kwa wanachama yatapungua kwa kiasi kikubwa ,endeleeni kujipanga vyema ,sisi kama Wizara tuna imani na utendaji wenu.”
Ameutaka Mfuko huo kuendelea kuboresha huduma na kuwafikia wanachama waliopo vijijini ili nao waweze kufurahia ustaafu wao popote walipo badala ya kuwaacha wastaafu waendelee kufunga safari mpaka makao Makuu ya mkoa kwa ajili ya kusaka huduma za Mfuko .
Awali Mkurugezni Mkuu wa PSSSF CPA Hosea Kashimba alisema,makuabalino hayo yanaenda kushughulikia michango ambayo haikuwasilishwa katika uliokuwa Mfuko wa PSPF kwa jina maarufu ‘Pre 199 liability’.
CPA Kashimba amemshukuru Rais Samia kwa kushughulikia suala hilo ambalo limekuwepo kwa muda mrefu na kupatiwa ufumbuzi chini ya utawala wake.
Aidha alisema,uwekezaji huo wa Serikali utasaidia Mfuko kupata mapato yanayotokana na hati fungani kwa takribani shilingi bilioni 120 kwa mwaka huku akisema pia wanaamini utekelezaji wa jambo hilo utawezesha Mfuko kupata unafuu wa deni la Pre 1999 na pia kuuwezesha kutimiza jukumu lake la msingi la kulipa mafao.
More Stories
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba
TRA kuongeza idadi ya waendesha uchumi walioidhinishwa
TRA Tanga wajivunia ukusanyaji mapato