Na Esther Macha,Timesmajira,Online, Mbeya
SERIKALI ya awamu sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imetenga shilingi bilioni.6.1 kwa ajili ya wanasayansi ili waweze kufanya tafiti ngumu ambazo zitaleta ubunifu ndani ya nchi.
Hayo yamesemwa leo na Naibu waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto,Dkt.Godwin Molleli wakati wa kufunga kongamano la wanasayansi la kitaifa kuhusu vvu na ukimwi katika maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani ambayo kitaifa inafanyika mkoani mbeya ambapo mgeni atakuwa Rais Samia .
Dkt.Molleli amesema kwamba Rais Samia ana mwelekeo ambao anataka nchi iende kwa mwendo wa wanasayansi ambapo itasaidia watanzania waweze kufanya vitu ambavyo vimebuniwa na wanasayansi ndani ya nchi.
“Leo nimekuja kufunga kongamano hili lakini naomba niwahamasishe kwa pamoja kufanya tafiti na kuangalia takwimu na kusaidia masuala ya kila siku na kujua mwelekeo lakini ni wakati mwafaka wa dunia tuanze na sisi kugundua”amesema Naibu waziri .
Akizungumzia kuhusu dawa za ukimwi kutengeneza usugu Dkt.Molleli amesema kwamba serikali imeanza kutengeneza mfuko kwa ajili ya kujitegemea.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa utafiti chuo kikuu cha Muhimbili Prof.Bruno Sunguya amesema kuwa watafiti pamoja wadau wa maendeleo wamefikiri kwa pamoja changamoto mbali na namna ya kuzitatua na kuongeza tija.
“Lakini pia Naibu waziri wa afya ametupa changamoto namna ya kuongeza ubunifu kama watafiti tumechukua na tutafanyia kazi kwa kushirikiana na wadau ,lakini pia tumeweza kuzungumzia ongozeko la maambukizi mapya kwa vijana na watoto wadogo ,tutaendelea kushirikiana na serikali kubuni miradi ya ukimwi na vvu ambayo inaweza kutekelezwa kwa ubunifu zaidi “amesema Prof .Sunguya.
Akizungumza wakati wa ufungaji wa Kongamano hilo Mkurugenzi wa tume ya kuthibiti ukimwi Tanzania (TACAIDS)Dkt. Leonard Maboko amesema kwamba wamekuwa wakichukulia kwa uzito masuala ya ukimwi na kwamba kama watafiti wataendelealea kufanya tafiti mbali mbali ili kuweza kushirikiana na serikali .
More Stories
CP.Wakulyamba ashuka Katavi na Nguzo nne za Uongozi
Zanzibar kuzalisha wachezaji wenye vipaji
Maandalizi ya mkutano mkuu CCM yapamba moto