May 15, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Upatikanaji taarifa sahihi za uvuvi mdogo wasisitizwa

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online. Morogoro

SERIKALI kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi imesisitiza upatikanaji wa taarifa sahihi za uvuvi mdogo nchini kwa kuangaza taarifa za wavuvi wadogo zilizofichika ili ziweze kutumika kwa mipango ya maendeleo endelevu kwa lengo la kukuza Uchumi.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Uvuvi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye hotuba yake ya ufunguzi wa warsha ya wadau wa sekta ya uvuvi ya kupitia matokeo ya utafiti wa mchango wa Uvuvi mdogo iliyosomwa kwa niaba yake na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti, Mafunzo na Ugani (DRTE) Dkt. Erastus Mosha mjini Morogoro meishoni mwa wiki.

Akisoma hotuba hiyo, Mkurugenzi huyo amewakumbusha wadau kuwa uvuvi ni sayansi, hivyo usimamizi wa rasilimali.