SERIKALI yaombwa kutumia tafiti katika shughuli zake
Na Stephen Noel – Mpwapwa.
SERIKALI imeombwa kuzitumia tafiti mbalimbali zinazofanywa na taasisi za kiserikali na zisizo za kiserikari nchini kwa lengo la kupatia majawabu ya changamoto zinaikabili Jamii kwa sasa.
Kauli hiyo imetolewa na Jana na Mkurugenzi wa Taasisi ya isiyo ya kiserikali ya RELI(Regional Education Learning Initiative) Pendo Maisel alipokuwa akiongea na wazazi na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya mount Igovu Katika uzinduzi wa taarifa ya utafiti uliofanywa na shirika hilo.
Maiseli amesema shirika hilo limejikita kuijengea uelewa Jamii katika masuala ya Afya,Elimu,Uchumi na ulinzi nausalama wa mtoto pamoja kupinga ukatili wa kijinsia.
Katika utafiti uliofanywa katika wilaya ya Mpwapwa na Shirika hilo ambao uliangazia masuala ya kiwango cha uelewa wa vijana Katika masuala tofauti tofauti ,amesema viwango vya kujitambua na kudhibiti hisia utafiti ulibaini kati ya vijana 10 ni vijana wanne waliweza kuwa na uelewa wa kiwango cha Moja cha utatuzi wa kujitambua na kudhibiti hisia ambacho ni kiasi cha chini kabisa.
Amesema katika masuala ya kujitambua utafiti ulibaini asilimia kubwa ya vijana walionekana Kati ya vijana 10 ni vijana 5 walionekana kujitambua na katika suala la heshima utafiti ulibainisha asilimia 49.9 ya vijana wana heshima.
Adha amesema katika umahiri wa matumizi ya kidigitali utafiti ulibaini aslimia 71 ya vijana hawezi kutumia digitali wakati asilimia 19 wanatumia kwa shida na asilimia 10 waliweza kutumia kirahisi.
Amesema utafiti huo ulilenga kuanzia masuala makuu manne ambayo ilikuwa ni kuangalia ulewa wa vijana Katika kujitambua ushirikiano,utatuzi wa matatizo na kiwango cha heshima Kwa Jamii pamoja stadi za Maisha kudhibiti hisia na matumizi ya digitali.
Akifungua utafiti huo Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa, Sophia Kizigo amesema nchi zote zilizoendelea zimetumia tafiti mbalimbali Katika kuondoa Changamoto za Jamii .
Amesema kuwa serikali amekuwa ikitumia tafiti zinazofanywa na taasisi za serikali na zisizo za serikali katika kuleta majawabu ya changamoto za Wananchi.
Msimamizi wa utafiti huo, Johaiven Bikongolo ambae ni muhadhiri msaidizi Katika chuo ckikuu cha Mt. John amedai kuwa Katika wilaya ya Mpwapwa walifanya utafiti Kwa vijana kati ya Miaka 13-17 na jumla ya kaya 361 zilifikiwa wakiwemo vijana nje ya shule na vijana ndani ya shule na jumla ya vijana 442 walifikiwa.
Mwisho.
More Stories
Mjumbe wa Baraza UWT ahimiza wananchi kuwachagua viongozi wa CCM
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â