Na Bakari Lulela
IMEELEZWA kuwa Serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ndio iliyowapa fursa Wamachinga jukumu la kutekeleza kazi za kuratibu , kuwaelimisha na kuhakikisha wanatoka maeneo yasiyo rasmi na kupangiwa maeneo mengine.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkoani humo Mwenyekiti wa Machinga Mkoa wa Dar es Salaam, Steven Lusinde amesema viongozi wa Machinga chukueni maelekezo ya Rais katika kuwaelimusha, kuwapanga na kuwaratibu watu wenu.
“Tulipata maelekezo kutoka kwa viongozi wa juu septemba 10 mwaka huu ilituamuru kuendesha zoezi la kuwapanga vema wafanyabiashara wadogo kutoka maeneo yasiyo rasmi na kuwapeleka maeneo mengine,”amesema Lusinde
Aidha Mkuu huyo amesema kwamba kutoka na utaratibu kama viongozi wamebaini baadhi ya kasoro zinazotoka na uchache wa maeneo ukilinganisha na halisi na idadi ya watu wanaotarajia kuelekea maeneo hayo.
Kiongozi huyo wa Machinga ameiomba menejimenti na Serikali kuhakikisha wanafanyakazi kwa ushirikiano ili kuondoa sintofahamu miongoni mwa wafanyabiasha.
Kwa kuwa Machinga wapo katika hatua za mwisho za usajili wa taasisi yao, wameitaka Serikali kuwa nao bega kwa bega katika m ajukumu mbalimbali ya kitaifa ya kibiashara yatakayompa mfanyabiashara mwanya wa k upata uhalali kwenye huduma za Bima za afya,Umeme na maji.
Wito umetolewa kwa wafanyabiashara kuendelea kuzingatia sharia na taratibu zilizotolewa na Serikali ili kufikia malengo kusudiwa kwa kumtoa Mmachinga toka kwenye biashara ndogo hadi biashara kubwa.
More Stories
Waziri Mkuu: Tumieni matokeo ya tafiti za kisayansi katika utekelezaji wa mipango ya kitaifa
Zaidi ya wananchi 32,000 Vijiji vya Wilaya za Morogoro na Mvomero kuanza kupata mawasiliano
Wafanyabiashara waomba elimu ya namna watakavyorejea soko kuu