Na Bakari Lulela,Timesmajira
SERIKALI ya jamhuri ya muungano wa Tanzania imesema kuwa chama cha wataalamu wa menejimenti ya kumbukumbu na nyaraka (TRAMPA) ni injini kwa watumishi wa umma ambao ni wabeba maono ya rasilimali watu na jamii ya watanzania.
Akizungumza jijini Dar es salaam kwenye ufunguzi wa mkutano wa 13 wa chama hicho uliofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee mgeni rasmi waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa Majaliwa amewapongeza viongozi na wanatrampa kwa kuhudhuria kwa umoja huo.
“Chama cha TRAMPA kimebeba dhamana ya nchi hii kwa kuandaa na kuhifadhi nyaraka mbalimbali za kitaalamu ambayo ni maono ya serikali katika kuuongoza umma wa watanzania,” amesema Majaliwa

Aidha Majaliwa ameeleza kuwa chama cha TRAMPA kimekuwa na malengo mbalimbali ikiwemo uwajibikaji na utawala bora , utunzaji wa nyaraka mbalimbali za kitaalamu ambazo watumishi wa umma ni rasimali itakayowezesha kuleta maendeleo ndani ya jamii yetu.
Hata hivyo Waziri mkuu aliahidi kuchangia kiasi cha shilingi milioni kumi ya harambee ya uchangiaji ujenzi wa jengo la Ofisi ya TRAMPA inatarajia kujengwa katika jiji la Dodoma.

Kwa upande wake Waziri wa nchi Ofisi ya Raisi menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora George Simbachawene alieleza kwamba serikali itaendelea kushirikiana kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wanatrampa ambao ndio nguzo kubwa kwa watumishi wa umma.
Simbachawene amesema kwamba wataalamu hao wamekuwa ni hazina katika kufanya kazi ya kujenga nchi pamoja na kulinda ubora na maarifa ya nguvu kazi ya Taifa hili kwa maendeleo ya watanzania.

Nae mwenyekiti wa chama hicho Devotha Mlope ameeleza changamoto mbalimbali zinazokikabili chama ni pamoja na ujenzi wa miundombinu ya Ofisi katika eneo maalumu lilipo katika mji wa serikali Dodoma.
Mwenyekiti huyo amefafanua kuwa TRAMPA ina jumla ya wanachama elfu 80 na imekuwa ikiendesha programu mbalimbali kwa wafanyakazi wa umma kwa lengo la kupata ujuzi na maarifa kwa sekta mbalimbali.

More Stories
Bilioni 7 kuwainua vijana 308 sekta ya uvuvi
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako