December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Serikali yachunguza juu ya wanafunzi kufundishwa vitendo kinyume na maadili

Na Mwandishi wetu, Timesmajira Online

SERIKALI imetuma timu maalum kwenda mkoani Kilimanjaro kuchunguza tuhuma juu ya taarifa kuhusu wanafunzi kufundishwa vitendo vilivyo kinyume na maadili katika baadhi ya shule mkoani humo kama ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari mwanzoni mwa wiki hii.

Akizungumza na Waandishi wa Habari katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma,Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda amesema timu hiyo inaongozwa na kamishna wa elimu nchini, Mwanasheria wa Wizara na Mkurugenzi wa Uthibiti Ubora.

“Tumeshtushwa sana na jambo hilo,tumelichukua suala hili kwa umuhimu mkubwa tumeongea na mkuu wa mkoa na kama kuna jinai yeyote basi hatua za kisheria zichukuliwa mara moja.”

Amesema Waziri Mkenda.Prof,Mkenda amesema kwamba timu hiyo imeasha anza ‘uchunguzi’ katika shule zilizotajwa na hatua za haraka zitachukuliwa kwa wahusika wote watakaobainika kuhusika na kadhia hiyo.

Waziri Mkenda ameongeza kuwa wizara ya Elimu itatoa namba maalumu ili kuwezesha wananchi kutoa taarifa za vitendo hivyo vinavyochafua taswira ya elimu,kuondoa Imani ya wazazi kwa shule na inaharibu vijana ambao ndiyo nguvu kazi ya taifa.

“Katibu Mkuu atatangaza namba ambayo mtu yeyote akijua kuna vitendo kama hivyo kwenye shule au chuo chote nasi tutaifanyia kazi kwa kufanya uchunguzi ili kudhibiti vitendo hivyo” ameeleza Prof.Mkenda.Prof.Mkenda

ameongeza kuwa katika kuweka mipango endelevu ya kudhibiti vitendo hivyo Wizara ya Elimu,Sayansi na teknolojia inashirikaina na wizara nyingine za kisekta katika kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsi katika jamii ikiwemo maeneo ya shule na vyuo nchini.