May 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Dkt. Biteko: Mradi wa JNHPP kukamilika Desemba 24

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online

NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt Doto Biteko amesema Serikali imesema imeanza uzalishaji wa umeme kupitia mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia maji wa Julius Nyerere (JNHPP) wenye uwezo wa kuzalisha Megawati 2,115, ambapo uzalishaji huo umeanza kwa Megawati 235 kupitia mtambo namba tisa.

Dkt Biteko ameyasema hayo Bungeni jijini Dodoma wakati akisoma hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Nishati kwa mwaka wa fedha 2024/2025.

Amesema Matarajio ya mradi huu ni kukamilika Desemba 2024 kwa mitambo yote nane yenye uwezo wa kuzalisha Megawati 235 kila moja kuwa inazalisha umeme”. amesema Dkt. Biteko