Na Ashura Jumapili, TimesMajira Online,Biharamlo.
Serikali kupitia Wizara ya Afya imeanza kujenga kituo cha kudumu cha watu wenye maambukizi ya mlipuko,wilayanj Biharamulo mkoani Kagera,ili kupambana na magonjwa hayo,ikiwemo kituo cha mfumo wa hewa tiba pamoja na maabara jongezi.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Afya Jenesta Mhagama,katika hafla ya kutangaza hitimisho la ugonjwa wa Maburg,uliofanyika wilayani Biharamlo ambapo ndipo mlipuko wa Marburg ulitokea na kusababisha vifo vya watu wawili.

Anasema ili kuweza kujihakikishia kinga na udhibiti zaidi,Wilaya zote zilizopo mpakani vitajengwa vituo vya kudumu vya watu wenye maambukizi ya mlipuko pamoja na maabara jongezi.
Ametaja magonjwa yanayoaambukizwa kwa kasi ni ya mlipuko pamoja na magonjwa yasiyoambukiza yakiwemo ya moyo, figo, kisukari na mengine na kuwa Serikali imeishayawekea mkakati wa kuyadhibiti.
Asema, tangu alipofariki mgonjwa wa mwisho wa Maburg zimepita siku 42 hivyo Tanzania haina tena mlipuko wa Maburg, na kuutangazia umma na jamii ya kimataifa kuisha kwa mlipuko huo.
Kwa upande wake mganga mkuu wa serikali Daktari Grace Magembe ameeleza kuwa, Januari 16,2025 wizara ya afya ilipata tetesi za kuwepo wagonjwa wa ugonjwa usiojulikana katika kijiji cha Katera kata ya Ruziba wilaya ya Biharamlo mkoani Kagera.
Anasema tetesi hizo zilienda sambamba na watu ambao walipoteza maisha kwa nyakati tofauti tofauti kama nane hivi ikawa haijulikani ni kwa sababu gani kwa haraka walikuja kufanya utafiti wa awali na kuchukua sampuli wakapata mgonjwa mmoja na Januari 20,2025 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan aliutangazia umma uwepo wa ugonjwa wa Maburg.

Ambapo amesema,hadi kufikia Januari 28, mwaka huu waliokuwa wamepata maambukizi walikuwa ni watu wawili ambao wote walipoteza maisha lakini baada ya kupata taarifa hizo waliimalrisha timu ya uratibu ngazi ya kitaifa.
“Tulifanya ufuatiliaji Mkoa mzima wa Kagera na kupata watu 281,ambao walikuwa wametengamana na wale wagonjwa ambao tuliwaibua miongoni mwao 64 walikuwa ni watumishi wetu wa afya, watu hao waliwekwa karantini na kufikia Februari 10, mwaka huu wote walitoka karantini salama na kuendelea na shughuli zao,”amesema Dkt Magembe.
Hata hivyo amesema walikumbana na changamoto ya unyanyapaa ambayo ilisababishwa na taarifa za uzushi ambapo ilionekana kwamba wananchi wakishaona mtu ameugua au alikuwa amewekwa karantini amerudi nyumbani wanaona kama vile hafai kuendelea kuishi na jamii.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Hajat Fatma Mwassa, amewataka wananchi wa Mkoa huo kuacha tabia ya kuwakaribisha wageni bila utaratibu na waache kujitibu kienyeji badala yake wanapougua waende hospitali wapate ushauri na matibabu ya madaktari.
Amesema ugonjwa umeisha lakini, waendelee kuchukua tahadhari kwa kuepukana na mikusanyiko isiyo ya lazima, kunawa mikono na kutumia vitakasa mikono.
More Stories
MSIGWA:Mfumo wa usajili waandishi wa habari kidijitali upo mbioni kukamilika
Kongani ya Viwanda ya Sino _Tan kutoa ajira laki moja
Waandishi wa habari kutambulika kidijitali