November 21, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Serikali yaahidi makubwa kongamano la uwekezaji Afrika mashariki 2024

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Serikali ya Awamu ya Sita imesema Ipo tayari kuunga mkono uwekezaji katika sekta ya urahisishaji wa miamala ya Kifedha ( FINTECH ) barani Afrika na kuona namna gani serikali inaweza kufanya kazi kwa urahisi na Makampuni yanayorahisisha makampuni ufanyaji wa miamala na kufanya gharama kuwa ndogo kwa Wananchi.

Hayo yamebainishwa na Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Bi. Sauda Msemo wakati akifungua Kongamano kubwa la wafanyabiashara Afrika Mashariki “East Africa Investment Forum’ lenye lengo la kuunganisha wafanyabiashara hususani watoa huduma za kifedha kwa njia ya mtandao kutoka nchi za Afrika Mashariki na Kati, Kingamano lililoandaliwa kwa ushirikiano na vyama vikuu vya FINTECH kutoka Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, na Tanzania, linalofanyika kwa Siku 2 ( Septemba 12-13 ).

Akizungumza baada ya Ufunguzi wa Kongamano ilo Katibu Mkuu Mtendaji wa Umoja wa Makampuni yanayotoa Huduma za Kifedha kupitia Teknolojia Tanzania ( TAFINA ) Bw. Shedrack Kamenya amesema zaidi ya Wawekezaji 10 wameshiriki Kongamano hilo , na lengo kubwa la kuwaleta pamoja watoa Huduma za Kifedha, Watunga Sera , Wawekezaji na wadau wa SEKTA ya Huduma za Kifedha barani Afrika limetimia

” Kauli mbiu yetu ni Wekeza na Ingia Ubia ” Invest and Partner ” katika utoaji wa Huduma za Kifedha, jukwaa hili limekusudia kupambanua mada mbalimbali katika eneo wa uwekezaji katika Huduma za Kifedha lakini pia tutaangazia mazingira ya kisera ambayo yatarahisisha upatikanaji wa Mitaji kwa watoa Huduma pamoja na upotevu wa fedha unaotokana na Uharifu wa Kimtandao ( Cyber Security ) na maeneo mengine kadha wa kadha ambayo tutaangazia ” amesema Bwn . Kamenya .

Kongamano ili linaendelea kwa siku mbili Septemba 12 & 13 Jijini Dar Es Salaam.

Kwa upande mwingine Mmoja wa Washiriki wa Kongamano hili la Kihistoria Bwn. Alfred Tembo amewapongeza TAFINA kwa kuwaunganisha pamoja katika Kongamano hilo .