Na Hadija Bagasha, TimesMajira Online, Tanga
Serikali ya Nchini Uganda imesema tayari imeshamaliza changamoto ya ardhi iliyokuwa ikiwakabili katika mradi wa ujenzi wa mafuta ghafi kutoka Hoima nchini humo hadi Chongoleani Tanga na kwamba hivi sasa kinachoendelea ni taratibu za kuchimba na kulaza mabomba kwenye maeneo ambayo mradi unapita.
Hayo yamesemwa na Waziri wa nchi anayeshugjulikia maendeleo ya madini kutoka wizara ya nishati na madini-Uganda wakati alipotembelea eneo la Chongoleani jijini Tanga ambapo kunajengwa matenki ya kuhifadhia mafuta ghafi kutoka Nchini Uganda kwajili ya kusambazwa kwenye maeneo mengine.
Waziri huyo aliyasema hayo wakati wa ziara iliyofanywa na ujumbe kutoka, nchini humo ilioambatana na wabunge wa Uganda, wataalamu mbalimbali wanahusika na masuala ya nishati na madini kutoka nchini humo na kuongozwa na Waziri wa madini wa nchini Uganda Peter Lokeris.
Amepongeza namna mashirikiano yaliyopo kati ya serikali ya Uganda na Tanzania mara baada ya kujionea maendeleo ya mradi huo kwa upande wa Tanzania na kueleza kuwa wataendelea kudumisha ushirikiano huo ulioanzishwa katika nyanja za kibiashara na uchumi kwa maslahi mapana ya pande zote mbili na kuzifanya nchi hizo kuwa kitomvu Cha maendeleo kwa wananchi wake .
“Tanzania ni eneo zuri na sahihi kwa uwekezaji wa kibiashara na kuweza kukuza uchumi , huu ni uchumi mkubwa mahusiano na makubaliano yote yaliyowekewa tutayafanyia kazi na kuzidi kuyaendeleza , tunafurahi Sana kuwa kwa Sasa kwa pande zote mbili za Kyle Uganda na hapa Tanzania tayari mradi huu umeshaaanza hii itazidi kufungua ufumi wetu” alisema Lakeris.
Sambamba na hayo alisema kuwa amani na utulivu uliopo ndani ya nchi ya Tanzania ni kivutiotosha cha kuweza kuwaleta wawekezaji mbalimbali na kuiwezeaha miradi mbambali kikubwa kuweza kutekelezwa hatua ambayo inazidi kuongeza uchumi wa wananchi mmoja mmoja na hata Taifa kwa ujumla.
Akizungumza katika ziara hiyo Katibu Mkuu wa wizara ya Nishati Felchesmi Mramba amesema tayari wananchi zaidi ya 600 wamelipwa fidia na wengine bado wanaendelea kulipwa ili kupisha ujenzi huo wa Bomba la mafuta.
Katibu Mramba amesema tayari zaidi yao 8800 waliopo kwenye maeneo yanayopitiwa na mradi huo na zaidi ya shilingi bilioni tano tayari zimeshalipwa.
Aidha Katibu Mramba alisema kuwa katika maeneo yenye vituo maalumu kwaajili ya mradi huo wananchi tayari wamehamishwa ikiwa ni pamoja na kulipwa fidia zao na kujengewa nyumba.
“Nataka niseme kwamba Kazi za fidia kwa wananchi wote waliopo kwenye eneo litakalopitiwa na mradi wa Bomba la mafuta zaidi ya Wananchi elfu 8800 maeneo yao yameshafanyiwa tathmini na wanasainishwa mikataba kwaajili ya kulipwa lakini wananchi 600 waliyokuwa na nyumba zao katika eneo lote ambalo Bomba litapita wamelipwa fidia na wengine wamejengewa nyumba na karibia bilioni 5 zimeshalipwa na nyingine zaidi zimeandaliwa kwaajili ya malipo” alisema Mramba.
Ujumbe wa kamati ya nishati na madini na maliasili ukiongozwa na waziri wa nishati na madini kutoka nchini Uganda umefanya ziara ya siku mbili mkoani Tanga kutembelea na kujionea maendeleo ya ujenzi wa Bomba la mafuta linalotoka Hoima Hadi Chongoleani Tanga Tanzania ambapo mradi huo unaotekelezwa na kamapuni ya mafuta ghafi ya Afrika Mashariki EACOP .
More Stories
Wakuu wa Wilaya,Wakurugenzi watakiwa kusimamia programu za chakula shuleni
Mbowe akuna wengi kuhusu maridhiano
Waziri Chana amuapisha Kamishna uhifadhi NCAA, ampa maagizo mazito