NA HERI SHAABAN( ILALA)
MWENYEKITI wa Serikali ya Mtaa Viwege Majohe wilayani Ilala,Amina Kapundi, amesema kipaumbele cha mtaa wa Majohe Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam kujenga kituo cha Polisi cha kisasa daraja B kwa nguvu za wananchi ambapo tofali 800 zimepatikana za kuanzia ujenxi huo.
Mwenyekiti Amina Kapundi, alisema hayo Mtaa wa Viwege katika kikao cha wananchi kwa ajili ya kuwashukuru na kuwatangazia na kuwatamburisha Kamati za Wajumbe na wasaidizi wake ambapo kila Kamati iliyotamburishwa ikiwemo kamati Afya,Elimu,Mazingira, na Ulinzi na usalama .
“Nawashuku wananchi kwa kukichagua Chama cha Mapinduzi CCM ambapo mimi na wajumbe wangu tumeshinda kwa kishindo katika uchaguzi wa Serikali za mitaa ccm imeshika dola naomba mniamini na wajumbe wangu tuweze kuleta maendeleo ambapo kipaumbele chetu cha kwanza kituo cha Polisi daraja B kitakuwa cha kisasa na mahabusu yake eneo lipo tayari litakalotumika kwa ajili ta ujenzi “alisema Amina
Amina Kapundi, aliwataka Wananchi wa Viwege na wadau wa Maendeleo kuchangia kwa hali na Mali ujenzi huo wa kituo cha Polisi daraja B kwani kutoa ni moyo sio usajili.
Alisema kituo hicho kikikamilika kitakuwa kinatumika Viwege na majohe yote pamoja kata za jirani kwani aliwatka wadau Wafanyabishara kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan za utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi na kujenga Tanzania ya uchumi wa viwanda .
Kwa upande wake Polisi Kata Majohe Ally Mntambo alisema sheria ndogo ya Serikali za Mtaa kila mwanachi anatakiwa kulinda au kuchangia tozo ya ulinzi kwa ajili ya kuimarisha usalama wa mtaa.
More Stories
Madiwani waomba Jimbo la Korogwe Vijijini ligawanywe
Dkt.Nchimbi:Watoa rushwa hawatakiwi CCM
Dkt.Diallo:Nunueni pembejeo mapema baada ya kuuza mazao