Na Heri Shaaban, TimesMajira Online
OFISI ya Serikali ya Mtaa Kalume kwa kushirikiana na Chama cha Mapinduzi Tawi la Shauri moyo, wamechanga shilingi milioni 1 kwa ajiii ya fomu ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan mwaka 2025
Fedha hizo shilingi milioni 1 ya fomu ya Rais Dkt.Samia amekabidhiwa Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Ilala Said Sidde ,wakati wa Semina ya Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya tawi la Shauri moyo kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa semina hiyo mtoa Mada mkuu alikuwa Mwenezi wa CCM wilaya ya Ilala Mwinyimkuu SANGARAZA.
Akizungumza katika mkutano huo mara baada kukabidhi fedha hizo Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Kalume Hajji Bechina, alisema kwa mapenzi mema ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Serikali ya Mtaa Kalume wanaunga mkono juhudi zake Rais aendelee kuchukua fomu hivyo kwa kushirikiana tawi wanachanga milioni moja ya Fomu.
“Rais Dkt.Samia amefanya mambo makubwa katika uongozi wake wanajivunia utekelezaji wa Ilani ya chama vizuri Ilala fadha za Rais utekelezaji wa Ilani umeweza kujenga vituo vya afya zahati sekta ya Elimu shule na Barabara na masoko “alisema Bechina.
Mwenyekiti Bechina aliwataka wananchi wake wa mtaa Kalume mwaka 2025 kuendelea kuwapigia kura viongozi wao waliopo madarakani Rais Samia suluhu Hassan, Mbunge Mussa Zungu, na Diwani Saady Kimji waweze kuendelea kuleta maendeleo
Mwenyekiti wa ccm wilaya ya Ilala Said Sidde alipongeza Hotuba ya Diwani wa Kata ya Ilala Saady Kimji ,ambapo aliwataka Ilala kuendelea kushikamana na kujenga Umoja na kuendelea kuchagua CCM.
Mwenyekiti Sidde alisema Rais Dkt.Samia ametoa fedha nyingi za miradi ya maendeleo Ilala kwa ushirikiano wa Mbunge Musaa Zungu na Diwani Saady Kimji mikakati iliyopo sasa ya Serikali kujengwa soko la kisasa Ilala na Barabara za kisasa..
Mwenyenezi wa CCM wilaya ya Ilala Mwinyimkuu SANGARAZA alimpongeza Mwenyekiti wa Karume Haji Bechina kwa ushirikiano wake chama na Serikali pamoja na wananchi wake ambapo aliwataka waendelee na mahusiano mema na kuakikisha ccm ina shika dola.
Diwani kata ya Ilala Saady Kimji alisema dhumuni la mafunzo hayo kuwapa elimu kuelekea Serikali za mitaa ambapo alisema Kamati ya Siasa wilaya ya Ilala imekuja na mikakati mikakati mipya waunde Kamati za ushindi kwa ajili ya kujenga chama kiweze kushika dola .
More Stories
HGWT yawataka wazazi na walezi kulinda watoto dhidi vitendo vya ukatili
ACT-Wazalendo,waitaka Polisi kutobeba chama kimoja
Gavu aanika miradi iliyotekelezwa na Serikali ya awamu ya sita Geita