Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma
WIZARA ya Fedha Nchini ,imekutana na Washirika wa Maendeleo kwa ajili ya kujipima katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo hapa nchini ikiwa ni utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo inayoishia 2025 na kuweka mikakati ya Dira ya Taifa ijayo ya 2050.
Akizungumza katika kikao hicho kilicholenga kujadili maendeleo yaliyofanyika na kuweka mipango kuelekea Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050,Dkt.Juma Malik Akil amesema, Serikali imefanya jitihada mbalimbali katika kutengeneza urahisi wa utoaji huduma kwa wananchi.
“Kwa mfano matengenezo yaliyofanywa katika bandari ya Dar es Salaam ili kuruhusu ‘movement’ za huduma za usafiri kati ya Tanzania na nchi nyingine katika kusukuma uchumi.”
Vile vile amesema ,maendeleo mengine ni uwepo wa treni ya mwendokasi (SGR) ambayo haikuwepo miaka miwili iliyopita na kwamba bado Serikali inaendelea katika hatua ya kueiendeleza kwani bado haijakamilika.
Dkt.Akil amesema,pia Serikali inaendelea na ujenzi wa miundombinu mbalimbali ikiwemo ujenzi wa Bwawa la kuzalisha umeme la Mwalimu Nyerere ambalo baada ya kukamilika litachochea vivutio vya uchumi .
“Haya ndiyo tumeyafanya ikilinganishwa na tulipozungumza kipindi kilichopita tukiwa na washirika wetu wa Maendeleo ,n ani vitu ambavyo vinaonekana na kila mmoja.”amesisitiza Dkt.Akil
Kwa upande wake Naibu Katibu Mtendaji Tume ya Mipango anayeshughulikia Mipango ya Kitaifa Dkt.Mursal Milanzi alisema wawamekuwa wakishirikiana na Washirika hao wa Maendeleo ambapo jukumu la washirika hao wa Maendeleo kazi yao ni gkusaidia kwenye upande wa kiufundi na kifedha.
Dkt.Milanzi ambaye pia ni Kaimu Katibu Mtendaji Tume ya Mipango ,Wizara ya Fedha alisema wanapokuta kwenye mikutano kama hiyo wanajadiliana kitu gani kifanyike kwa miaka inayofuata.
“Kwa hiyo kimsingi tunakubaliana vipaumbele vya nchi , nchi inasema inataka kuchukua mwelekeo gani ambapo na wao sasa wanaangalia vipaumbele vyao kwa nchi zao ili ziweze kufanana na vipaumbele vyetu na baada ya hapo tuingie kwenye utekelezaji .”amesema Dkt.Milanzi na kuongeza kuwa
“Sisi Tume ya Mipango kwa siku ya leo tulipewa jukumu la kuzungumza kuhusu mwelekeo wa Dira mpya ya 2050 ,kama mnavyofahamu kwamba tumekuwa tukitekeleza Dira ya 2025 ambayo ilianza utekelezaji wake mwaka 2000 na 2025 ndiyo mwaka wa mwisho,
“Kwa sasa tumebakiwa na mpango mmoja wa mwaka mmoja kukamailisha utekelezaji wa Dira ya 2025 ,hivyo basi Mpango utaanza kutekelezwa 2026/2027.”
Aidha ameongeza kuwa “Katika utekelezaji wa Dira ya 2025 tumeona mafanikio kadhaa yaliyopatikana , tunashuhudia sasa huduma za afya ,miundombinu ya usafirishaji na miundombinu ya uzalishaji umeme imeboreka ,yote hiyo ni utekelezaji wa Dira ya 2025.”
Hata hivyo amesema,katika utekelezaji huo wa Dira ya Taifa 2025 kumekuwa na changamoto mbalimbali ambazo zimewafanya washindwe kukamilisha yale mambo ambayo waliyapanga wakati wameanza kutekeleza Dira hiyo.
“Kwa hiyo tunapokwenda sasa kwenye utekelezaji wa Dira ya 2050 tunaangalia kule tulikotoka tulitekeleza vipi na tunapokwenda tunatakiwa tutekeleze vipi,kwa hiyo kimsingi ujumbe ambao tulitaka kuutoa kwa wenzetu ni kwamba tuna vipaumbele ambavyo tayari vimejitokeza kwenye Dira ya 2050 ,kwa hiyo huo ndiyo mwelekeo ambao tunauona kwamba utakwenda kutusaidia katika nchi yetu.”
Dkt.Milanzi ametaja baadhi ya maeneo hayo kuwa ni Pamoja kuchagua miradi ambayo itakwenda kusaidia kukuza ajira ,kupata fedha za kigeni huku akisema itaisadia nchi kuinua sekta nyingine kama vile sekta ya kilimo na Viwanda.
Eneo lingine alisema ni la matumizi mazuri ya nafasi ya kijiografia ambapo Tanzania imekuwa ni nchi ambayo inasaidia kwenye masuala ya usafirishaji kwa nchi zinazopakana nazo zikiwemo Congo ,Zambia na Malawi ambazo zinatumia Bandari na barabara za Tanzania kusafirisha bidhaa zao.
“Kwa hiyo sasa tunajaribu kujitathimini kwamba ,je hii nafasi yetu ya kijiografia tumeitumaije ,tunaona kabisa Dira ya 2025 tumeitumia lakini tunadhani hatujaitumia vizuri zaidi ,hivyo tuna nafasi kwa Dira ya 2050 kufanya vizuri zaidi na kufaidika na eneo letu la kijiografia.”
Vilevile amesema eneo la madini ni muhimu kuangaliwa katika Dira ijayo ili kutoa fursa kwa nchi kunufaika na eneo hilo .etu ina madini huku akitaka madini hayo yatumike vizuri ili nchi iweze kupata fedha za kutekeleza miradi mingine.
“Pato ambalo tunalipata kwenye madini tunaweza kutengeneza ajira nyingi ,sasa tunazitumiaje tunapokwenda 2050 ,
“Nchi katika ngazi zote tujaribu kuiona dira haii kma chombo cha kutuletea maendeleo,hivyo wote tuna wajibu wa kuhakikisha kwamba Dira yetu inatekelezwa ipasavyo na mpaka kipindi hicho nchi yetu itakuwa imepiga hatua kubwa sana.”amesistiza Dkt.Milanzi
———- Forwarded message ———
From: joyce kassiki<jyckasiki@gmail.com>
Date: Fri, Feb 21, 2025, 15:38
Subject: Dira ya 2050 yawekewa mkakati wa utekelezaji
To: <majira2006@gmail.com>, <reubenkagaruki1970@gmail.com>
Na Joyce Kasiki,Dodoma
WIZARA ya Fedha na Mipango Nchini ,imekutana na washirika wa Maendeleo kwa ajili ya kujipima katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo hapa nchini ikiwa ni utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo inayoishia 2025 na kuweka mikakati ya Dira ya Taifa ijayo ya 2050.
Akizungumza katika kikao hicho kilicholenga kujadili maendeleo yaliyofanyika na kuweka mipango kuelekea Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050,Dkt.Akil alisema, Serikali imefanya juhudi katika kutengeneza urahisi wa utoaji huduma kwa wananchi.
“Kwa mfano matengenezo yaliyofanywa katika bandari ya Dar es Salaam ili kuruhusu ‘movement’ za huduma za usafiri kati ya Tanzania na nchi nyingine katika kusukuma uchumi.”
Vile vile alisema ,maendeleo mengine ni uwepo wa treni ya mwendokasi (SGR) ambayo haikuwepo miaka miwili iliyopita na kwamba bado Serikali inaendelea katika hatua ya kueiendeleza kwani bado haijakamilika.
Dkt.Akil alisema,pia Serikali inaendelea na ujenzi wa miundombinu mbalimbali ikiwemo ujenzi wa Bwawa la kuzalisha umeme la Mwalimu Nyerere ambalo baada ya kukamilika litachochea vivutio vya uchumi .
“Haya ndiyo tumeyafanya ikilinganishwa na tulipozungumza kipindi kilichopita tukiwa na washirika wetu wa Maendeleo ,n ani vitu ambavyo vinaonekana na kila mmoja.”alisisitiza Dkt.Akil
Kwa upande wake Naibu Katibu Mtendaji Tume ya Mipango anayeshughulikia Mipango ya Kitaifa Dkt.Mursal Milanzi alisema wawamekuwa wakishirikiana na Washirika hao wa Maendeleo ambapo jukumu la washirika hao wa Maendeleo kazi yao ni gkusaidia kwenye upande wa kiufundi na kifedha.
Dkt.Milanzi ambaye pia ni Kaimu Katibu Mtendaji Tume ya Mipango ,Wizara ya Fedha alisema wanapokuta kwenye mikutano kama hiyo wanajadiliana kitu gani kifanyike kwa miaka inayofuata.
“Kwa hiyo kimsingi tunakubaliana vipaumbele vya nchi , nchi inasema inataka kuchukua mwelekeo gani ambapo na wao sasa wanaangalia vipaumbele vyao kwa nchi zao ili ziweze kufanana na vipaumbele vyetu na baada ya hapo tuingie kwenye utekelezaji .”alisema Dkt.Milanzi na kuongeza kuwa
“Sisi Tume ya Mipango kwa siku ya leo tulipewa jukumu la kuzungumza kuhusu mwelekeo wa Dira mpya ya 2050 ,kama mnavyofahamu kwamba tumekuwa tukitekeleza Dira ya 2025 ambayo ilianza utekelezaji wake mwaka 2000 na 2025 ndiyo mwaka wa mwisho,
“Kwa sasa tumebakiwa na mpango mmoja wa mwaka mmoja kukamailisha utekelezaji wa Dira ya 2025 ,hivyo basi Mpango utaanza kutekelezwa 2026/2027.”
Aidha aliongeza kuwa “Katika utekelezaji wa Dira ya 2025 tumeona mafanikio kadhaa yaliyopatikana , tunashuhudia sasa huduma za afya ,miundombinu ya usafirishaji na miundombinu ya uzalishaji umeme imeboreka ,yote hiyo ni utekelezaji wa Dira ya 2025.”
Hata hivyo alisema,katika utekelezaji huo wa Dira ya Taifa 2025 kumekuwa na changamoto mbalimbali ambazo zimewafanya washindwe kukamilisha yale mambo ambayo waliyapanga wakati wameanza kutekeleza Dira hiyo .
“Kwa hiyo tunapokwenda sasa kwenye utekelezaji wa Dira ya 2050 tunaangalia kule tulikotoka tulitekeleza vipi na tunapokwenda tunatakiwa tutekeleze vipi,kwa hiyo kimsingi ujumbe ambao tulitaka kuutoa kwa wenzetu ni kwamba tuna vipaumbele ambavyo tayari vimejitokeza kwenye Dira ya 2050 ,kwa hiyo huo ndiyo mwelekeo ambao tunauona kwamba utakwenda kutusaidia katika nchi yetu.”
Dkt.Milanzi ametaja baadhi ya maeneo hayo kuwa ni Pamoja kuchagua miradi ambayo itakwenda kusaidia kukuza ajira ,kupata fedha za kigeni huku akisema itaisadia nchi kuinua sekta nyingine kama vile sekta ya kilimo na Viwanda.
Eneo lingine alisema ni la matumizi mazuri ya nafasi ya kijiografia ambapo Tanzania imekuwa ni nchi ambayo inasaidia kwenye masuala ya usafirishaji kwa nchi zinazopakana nazo zikiwemo Congo ,Zambia na Malawi ambazo zinatumia Bandari na barabara za Tanzania kusafirisha bidhaa zao.
“Kwa hiyo sasa tunajaribu kujitathimini kwamba ,je hii nafasi yetu ya kijiografia tumeitumaije ,tunaona kabisa Dira ya 2025 tumeitumia lakini tunadhani hatujaitumia vizuri zaidi ,hivyo tuna nafasi kwa Dira ya 2050 kufanya vizuri zaidi na kufaidika na eneo letu la kijiografia.”
Vilevile alisema eneo la madini ni muhimu kuangaliwa katika Dira ijayo ili kutoa fursa kwa nchi kunufaika na eneo hilo .etu ina madini huku akitaka madini hayo yatumike vizuri ili nchi iweze kupata fedha za kutekeleza miradi mingine.
“Pato ambalo tunalipata kwenye madini tunaweza kutengeneza ajira nyingi ,sasa tunazitumiaje tunapokwenda 2050 ,
“Nchi katika ngazi zote tujaribu kuiona dira haii kma chombo cha kutuletea maendeleo,hivyo wote tuna wajibu wa kuhakikisha kwamba Dira yetu inatekelezwa ipasavyo na mpaka kipindi hicho nchi yetu itakuwa imepiga hatua kubwa sana.”alisistiza Dkt.Milanzi
More Stories
Vitongoji Musoma vijijini vyaendelea kuunganishiwa umeme
Mpango mahsusi wa Taifa kuhusu Nishati wajadiliwa
Mwenyekiti CCM, Mbunge Rorya wavuruga mafunzo ya makatibu