Na Mwandishi wetu, Timesmajira Online
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. John Jingu amesema Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo inatafuta ufumbuzi wa changamoto mbalimbali kuhusu usawa wa kijinsia ili kujenga jamii yenye mlengo huo.
Dkt. Jingu ameyasema hayo (Aprili 14,2023) wakati akizungumza na Mkurugenzia Mkazi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) Wellington Chibebe ambapo pamoja na mambo mengine, wame kubaliana kuendeleza ushirikiano katika maeneo ya Ustawi wa Jamii, tiba mbadala ya Afya ya Akili, kuwawezesha wafanyakazi wasaidizi wa nyumbani na kuandaa mazingira wezeshi na bora katika sekta zisizo rasmi.
Dkt Jingu ameishukuru ILO kwa msaada wa kiufundi na kifedha katika Miradi ya Kuleta usawa (GEP) na katika utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) na uaandaji wa MTAKUWAA awamu ya II.
Kwa upande wake, Mkurugenzia Mkazi wa ILO, Wellington Chibebe ameishukuru Wizara kwa ushirikiano wanaounyesha kwao na ameahidi kuhakikisha wanashrikina zaidi katika kuijenga jamii bora.
Wellington Chibebe ameambatana Mratibu wa masuala ya Jinsia wa Shirika hilo Chiku Semfuko.
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa