Na Joyce Kasiki,Dar Es Salaam
SERIKALI inaendelea kusogeza huduma za kimahakama karibu na wananchi kwa kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ya ujenzi wa mahakama za Mwanzo hadi Vituo Jumuishi katika wilaya na Mikoa mbalimbali hapa nchini.
Mhandisi Ujenzi Andrew Weja kutoka Kitengo cha Usimamizi wa Majengo ya Mahakama (Maboresho) ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam katika maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba).
Amesema Kitengo cha Maboresho ndani ya Mahakama ndicho kinashughulika na miradi ya ujenzi wa Mahakama ambapo ndani yake kunakuwa na miradi ya ukarabati na ujenzi wa majengo mpya.
“Maboresho haya kwenye Muhimili wa Mahakama, yanalenga kusogeza huduma karibu na wananchi kwa kuwa majengo ya Mahakama kipindi cha nyuma hali haikuwa nzuri kama yanayojengwa na kuboreshwa sasa.
Amesema,kwa sasa kuna miradi ya ujenzi inaendelea ya mahakama za Mwanzo ,wilaya,mkoa,Mahakama Kuu na vituo Jumuishi huku akisema ipo baadhi ya miradi ya vituo Jumuishi vya utoaji Haki imeshakamilika na umedhaanza kutoa huduma kwa wananchi.
Kwa mujibu wa Mhandisi Weja, ituo hivyo vimejengwa Mikoa ya Dar Es Salaam (Temeke na Kinondoni),Arusha,Mwanza,Morogoro na Dodoma ambayo inakuwa ni jengo moja lakini ndani yake kunakuwa na huduma kuanzia mahakama ya Mwanzo,wilaya ,mpaka Mahakama Kuu.
Vile vile amesema ipo miradi inayoendelea kutekelezwa ya ia kuna miradi ya ujenzi wa vituo Junuishi vya utoaji haki ambayo inaendelea katika Mikoa mbalimbali ikiwemo Mikoa ya Singida, songwe,Katavi ,Songea ,Njombe, Lindi lakini pia mahakama za Mwanzo ,mikoa na wilaya zinajengwa katika Mikoa mbalimbali nchini
“Kwa hiyo tunaamini kwamba majengo ya mahakama yakiwa mazuri ,hata utoaji wa haki nao utaendelea vizuri kwa sababu mtu anafanya kazi katika mazingira mazuri ,hata utendaji wake wa kazi nao unakuwa mzuri.”amesisitiza
Pia amesema katika dhana hiyo ya kusogeza huduma kwa wananchi imeanzishwa mahakama inayotembea ili kufuata mwananchi mahali alipo.
“Kwa hiyo lengo la Serikali na mikakati yake ni kuendelea kuongeza majengo ya Mahakama kuanzia mahakama za Mwanzo ,wilaya na Mahakama Kuu katika maeneo mbalimbali huduma Mahakama za Mwanzo ambazo zinahitaji angalau kila Kata kuwe na Mahakama ya Mwanzo
“Kila wilaya iwe na mahakama ya wilaya na mahakama Kuu kila mkoa iwe na mahakama kuu ili kupunguza msongamano mahakamani na kesi kushughulikiwa mapema.”
More Stories
TRA kuongeza idadi ya waendesha uchumi walioidhinishwa
TRA Tanga wajivunia ukusanyaji mapato
Wambura asikitishwa na makundi CCM Nyakato