Na Mwandishi Wetu,TimesMajira Online
MRADI wa ukarabati wa soko la samaki Feri umepangwa kutekelezwa kwa muda wa miezi saba na bila kuathiri shughuli za wafanyabiasharanikiwa ni pamoja na mapato ya Halmashauri ya Jiji na kuendelea kutoa huduma kwa wananchi kama kawaida kadri itakavyowezekana.
Ameyasema hayo jana Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Mashimba Ndaki kwenye Mkutano wa wadau wa sekta ya uvuvi juu ya hatua zitakazofuatwa katika ukarabati wa soko la samaki la Feri Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika mkutano huo Waziri Ndaki amesema kuwa Wizara yake imeandaa mpango wa uhamishaji wa watu kwa muda katika maeneo ya soko yatakayofanyiwa ukarabati.
“Wafanyabiashara katika kanda 1 na 2 watatambuliwa na kuhamishiwa maeneo ya muda yaliyoandaliwa.Mpango huu utahakikisha kuwa baada ya ukarabati wafanyabiashara waliohamishwa watarudishwa katika maeneo yao ya awali, amesema Waziri Ndaki.
Aidha Waziri Ndaki amesema miundombinu ya uvuvi hususan mialo na masokoni muhimu katikakuhakikisha kuwa mazao ya uvuvi yanakuwa bora na salama kwa ajili ya afya ya walaji na hivyo kupata masoko ya ndani na nje ya nchi.
Amesema miundombinu ya uvuvi inasaidia katika kudhibiti uvuvi na biashara haramu ya mazao ya uvuvi, ukusanyaji wa mapato mbalimbali ya Serikali na upatikanaji wa takwimu na taarifa sahihi za uvuvi.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anaeshuhulikia masualaya Uvuvi,Dkt.Rashid Tamatamah amesema kuwa mapato yatokanayo na soko la Feri ni kati ya Shilingi Milioni 135 hadi 150 kwa mwezi kutegemeana na hali ya uvuvi mwezi husika.
Vilevile amesema kuwa soko hilo limeweza kutoa ajira rasmi zipatazo 117 na ajira zisizo rasmi takribani 2,780 hata hivyo soko hilolimekuwa na watmuaji 10,000 kwa siku ukilinganisha na wakati wa ujenzi wa soko hilo ambapo liliwahudumia watumiaji 1,500 kwa siku.
More Stories
Mwanasiasa mkongwe afariki Dunia
Rais Samia Kuzindua Sera Mpya ya Elimu na Mafunzo
Jokate awapa tano vijana UVCCM maandalizi Mkutano Mkuu wa CCM