November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Serikali kufanya utafiti nchini nzima kubaini uwepo wa madini

Na David John ,Geita

WAZIRI wa Madini Anthony Mavunde amesema ,Serikali imedhamiria kufanya utafiti na kupata taarifa za uwepo madini katika maeneo yote nchini Ili kiwawezesha wachimbaji wa Madini kufanya kazi hiyo kwa uhakika.

Akizungumza kwenye maonesho ya sita ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini mkoani Geita 2023,Mavunde amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha utafiti huo unakamilika ifikapo 2030 kwa maana ya ndani ya miaka Saba kutoka hivi sasa .

Amesema hatua hiyo itawezesha wachimbaji kupiga hatua kubwa kwani hawatafanya kazi kwa kubahatisha hivyo mitajo Yao itaendelea kustawi siku hadi siku tofauti na hivi sasa mitajo ya wengi hupotea kwani wanaochimba katika maeneo ambayo hawana uhakika kama madini yanapatikana.
“Nchi yetu ina kilomita za mraba ukizipeleka kwenye ekari ina ukubwa wa eneo ekari milioni 233,sisi tumefanya utafiti wa kina katika eneo la asilimia 16 tu ya eneo la ukubwa wa ekari milioni 233 ,na humo tutatoa maeneo ya makazi,tutatoa maeneo ya mbuga za wanayama na maeneo ambayo hivi sasa shughuli za madini haziruhusiwi kufanyika lakini bado tunabaki na eneo kubwa sana ,

“Sisi kama wizara na timu yangu tumekubaliana kwamba kama asilimia 16 tu ya eneo ambalo limefanyiwa utafiti ndipo eneo ambalo tunakimbizana wote na ndio linachangia kuingiza fedha za kigeni kwa asilimia 56 ya mauzo yote ya bidhaa nje ya nchi,sekta ya madini inaongoza.”amesema Mavunde na kuongeza kuwa

“Mwaka uliopita tumeuza nje ya ncxhi bidhaa za madini zenye thamani ya dola bilioni 3.3 ,ukizipeleka kwenye madafu ni zaidi ya shilingi trilioni saba hii ni kwenye pato la Taifa lakini kwenye mapato ya kodi sekta ya madini inachangia asilimia 15 ya mapato ya kodi ya ndani,mwaka wa fedha uliopita tumechjangia shilingi trilioni 2,na fedha zilizozunguka kwenye masoko yote mwaka wa fedha uliopita ni sh trilioni 1.6 sasa tukajiuliza hivi tukiongeza eneo kubwa kufanya utafiti hii nchi itakuwa wapi .”

Aidha Mavunde amesema,utafiti huo utawezesha kuonesha maeneo yenye Maji,malighafi za utengenezaji wa mbolea na vitu vingine vingi ambavyo vyote kwa pamoja vileta ustawi nchini.

“Tukifanya utafiti tutakuwa nanuwezo wa kubaini miamba yenye Maji ambayo Serikali kupitia wizara ya maji itachimba visima na wananchi wengi watapata Maji na maisha ya watanzania yataboreka,

“Lakini pia kupitia Maji hayo tutaweza kuchimba mabwawa na wakulima watafanya kilimo Cha umwagiliaji na hivyo kulima mara mbili kwa mwaka na hivyo kuleta usalama wa chakula nchini “amesema

Vile vile Mavunde amesema utafiti huo itawesha kuonesha malighafi za kutengeneza mbolea bidhaa ambayo Serikali hitumiabfedha nyingi kiagiza tan 350,000 kwa mwaka ,kwa hiyo upatikanaji wa malighafi hiyo utashawishi wawekezaji wa Viwanda vikubwa vya mbolea nchini .

“Kwa hiyo hayo yote yatafanikiwa kwa upimaji ndiyoaana tunasema madini ni maisha yetu ,madini ni maisha na utajiri.”amesema na kuongeza kuwa

“Nataka niwahahkikishie ,Serikali tumejipanga Ili wananchi mliopo kwenye tasnia ya uchimbaji muingie kwenye utajiri wenu.”amesisitiza Mavunde

xxx

Na David John ,,Geita

“Nataka niwahakikishie ,Serikali tumejipanga Ili wananchi mliopo kwenye tasnia ya uchimbaji muingie kwenye utajiri wenu.”amesisitiza Mavunde