May 3, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mavunde aipa kongole GF Truck

Na David John ,Geita

WAZIRI wa Madini Anthony Mavunde ameishukuru na uipongeza Kampuni ya GF Trucks&Equipment inayojishughulisha na uuzaji wa magari,mashine na mitambo kwa ajili ya shughuli mbalimbali zikiwemo za uchimbaji Madini kwa kuona umuhimu wa kushirikiana na sekta ya madini hasa wachimbaji katika kuwapatia vifaa katika mfumo ambao utawezesha wachimbaji wengi kumiliki vifaa vitakavyosaidia katika shughuli za uchimbaji.

Akizungumza katika uzinduzi wa Ofisi ya GF Truck mkoani Geita,Mavunde amewaomba waendelee kutanua wigo na kuwezesha wachambiji wengi zaidi kupata vifaa hivyo ambavyo vitaleta tija kubwa katika Taifa.

“Na sisi kama Wizara ,kwa kuwa tunao mkakati wa kuhakikisha kwamba tunaongeza shuguli za uzalishaji wa madini hapa nchini wa kuongeza wigo mpana zaidi wa madini ya aina mbalimbali kwa tafiti ambazo tutakwenda kuzifanya .”amesema Mavunde

Aidha ametumia nafasi  hiyo kutoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Madini nchini (STAMICO) kusimamia makubaliano waliyoingia baina yao na GF Truck ya kuwasaidia wachimbaji wadogo ili waweze kunufaika na mpango mzuri wa TRUCK wa kupata magari,mitambo na mashine kwa ajili ya shughuli zao za uchimbaji.

“Mpango mliokuja nao ni mzuri mkitekeleza katika maeneo machache mliyokuja nayo itasaidia kurahisisha shughuli za uchimbaji.”amesema Mavunde

Awali Mkurugenzi Biashara GF Trucks &equipment Salman Kalman amewakaribisha wadau mbalimbali wakiwemo wachimbaji wa madini kupata huduma katika Ofisi zilizopo mkoani Geita.

Ametumia nafasi hiyo kumpongeza na kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutengeneza mazingira mazuri ya uwekezaji ambayo yanakwenda kuleta tija kwa wachimbaji,wananchi na Taifa kwa ujumla.

“Magari tuliyonayo ambayo baadhi tunawakabidhi wateja wetu ni  matunda mazuri ya serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hasaan kwa kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji ambapo hivi sasa tunajivunia kuwa kiwanda chetu kilichopo Kibaha mkoa wa Pwani ambacho ni kiwanda pekee hapa nchini kuunganisha magari ,

“Na Mwaka huu kiwanda chao kitaunganisha magari zaidi ya 1500 mwaka huu tulianza kufanya upanuzi wa kiwanda chetu kwa lengo la kuanza kuunganisha magari madogo .”