Na Daud Magesa,TimesMajira Online. Magu
SERIKALI imesema itendelea kupokea wawekezaji katika sekta mbalimbali na kuwasikiliza ili kutatua changamoto wanazokutana nazo ili kuwasaidia waweze kuwekeza na kufanya biashara katika mazingira mazuri.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Dkt. Maduhu Kazi, wakati akipokea majengo ys Shule ya Sekondari Salama na Chuo cha Ufundi vilivyojengwa na kiwanda cha kuchambua pamba cha Alliance Ginnery kwa gharama ya sh. milioni 330.
Dkt. Kazi amesema Serikali ya awamu ya tano, inahitaji wawekezaji wanaofahamu serikali na wananchi wanahitaji nini, lakini wawe wanaisaidia jamii inayowazunguka ili kuleta mandeleo yao.
Amesema milango ya TIC, muda wote ipo wazi ili kuhakikisha inakuwa na taarifa za kila mwekezakaji na kujua anakabiliwa na changamoto yoyote na kuitatua kwa wakati.
Mkurugenzi huyo amesema kwa sasa, wanatumia teknolojia ya kisasa kuwasiliana na wawekezaji pamoja na kutumia ofisi za kanda, ili kuhakikisha kila mfanyabiashara anawekeza katika mazingira salama yasiyo na usumbufu wala urasimu.
“Hiki kiwanda kimezingatia maagizo ya Serikali ya awamu ya tano, tunahitaji wawekezaji kama hawa ambao wanaisaidia jamii inayowazunguka si wawekezaji wanaokwenda kuchimba mashimo mawili ya choo, halafu wanasema wameisaidia jamii,” amesema Dkt. Kazi.
More Stories
Bei za mafuta Novemba 2024,zaendelea Kushuka
TARURA yaomba Mkandarasi aitwe
Ilemela yakusanya bilioni 3.7.robo ya kwanza