November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Serikali ipo tayari kushirikiana na NIC

Na Penina Malundo, timesmajira,Online

KAMISHINA  wa Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima Nchini (TIRA) Dkt  Baghayo  Saqware amesema serikali ipo tayari kushirikiana na Shirika la bima la Taifa (NIC)  kwa kuhakikisha inanawafikia wakulima, wafugaji, na wavuvi wote  nchini.

Dkt Saqware ameyasema hayo jana alipotembelea katika banda la NIC lililopo katika Maonesho ya Biashara ya kimataifa 46 yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Jijini Dar es salaam.

Amesema serikali imekuwa ikitegemea sana Shirika la  NIC katika kuendeleza soko katika maeneo ya bima ya kilimo, majengo, pamoja na bima mbalimbali.

Dkt Sqware amesema NIC ni wazoefu zaidi katika soko la bima kutokana na wao kuwa na mtaji mkubwa na wataalamu wa kutosha katika soko.

Mkurungezi wa Masoko na huduma kwa wateja NIC, Yesaya Mwakifulele akizungumza na waandishi wa habari.

“Ukizungumzia bima Tanzania hakuna namna unaweza kuisahau NIC kwa maana ya wataalamu, uzoefu pamoja na mtaji”amesema Dkt Sqware

Vilevile amesema  hivi karibuni NIC wamejikita katika bima ya kilimo ambapo amewapongeza kwa hatua hiyo na kuhaidi kuendelea kushirikiana nao .

“Tayari tumewapatia namba viongozi wa NIC ili waweze kuwasiliana na  viongozi wa wakulima na wafugaji hapa nchini ili waaze kuangalia ni kwa namna gani wanaweza kuwafikia zaidi na kuwapatia bima,amesisitiza 

Naye Mkurungezi wa Masoko na huduma kwa wateja NIC, Yesaya Mwakifulele amesema katika Maonesho hayo NIC imejikita katika ushiriki kikamilifu kwa kuhakikisha inatoa huduma mbalimbali kuhusu suala nzima la bima.

Amesema katika Maonesho hayo wamekuja na APP  ya NIC kigajani ambayo inamuwezesha mteja kupata huduma akiwa nyumbani bila ya kufika katika ofisi zao.

Baadhi ya wananchi wakipata maelezo kutoka.kwa Afisa wa NIC.

“Kupitia APP hiyo mteja anaweza kujihudumia kwa hatua chache tu ambayo ataweza kukata bima ya aina mbalimbali ikiwemo nyumba, gari.

Akizungumzia kuhusu suala nzima la madai amesema NIC imekuwa ikifanya  ulipaji huo   ndani ya siku saba tu iwapo  taarifa zote zikiwa sawa.

“Kwa sasa hatuna  madai yoyote ambayo ayajalipwa labda  yale ambayo taarifa zake aziko sawa”amesema Mwakifulele

Aidha amewataka  watanzania wote kwa ujumla  kufika  katika banda lao ili waweze kupata elimu pamoja na  huduma za uhakika za bima ambazo zitaweza  kumsaidia pale anapopata majanga.