March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Serikali inatambua kazi nzuri ya OSHA nchini 

Na Bakari Lulela,Timesmajira

MKUU wa wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza Amina Makilagi amesema Serikali inatambua kazi nzuri inayofanywa na wakala wa Usalama na Afya mahafali pa kazi (OSHA) ya kusimamia utekelezaji wa Sheria ya usalama na Afya mahafali pa kazi ya mwaka 2003 ambapo imewataka waajiri kutekeleza Sheria hiyo Ili kukabiliana na magonjwa na ajali katika sehemu za kazi.

Ametoa kauli hiyo kwenye Bonanza la OSHA la huduma kwa jamii (OSHA CSR Bonanza 2025 ) lililofanyika jijini Mwanza kwa lengo la kutoa msaada wa vifaa muhimu kwa wanafunzi wa chuo cha ufundi Mirongo ambao baadhi yao wanna Ulemavu mbalimbali.

Vifaa vilivyotolewa na OSHA kwa chuo hicho ni pamoja na kompyuta, vifaa Kinga pamoja na vifaa vya  michezo ikiwemo mipira na jezi za mpira wa miguu na mpira wa Pete.

Mkuu wa wilaya ambaye alikuwa mgeni rasmi wa tukio hilo,ameihakikishia OSHA ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yake yanayohusisha kuyatambua maeneo ya kazi kupitia usajili maalumu na kuyatembelea kwa ajili ya ukaguzi na ushairi wa kitaalamu juu ya uboreshaji wa mazingira ya kazi.

“Nitoe rai kwa waajiri na wafanyakazi nchini kusoma na kutekeleza Sheria Na. 5 ya usalama na Afya mahafali pa kazi ya mwaka 2003 kwani ni dhahirii kuwa Sheri hiyo ikitekelezwa ipasavyo katika maeneo ya kazi hakutakuwa na ajali wala magonjwa na hivyo kupelekea maeneo ya kazi kuwa na uzalishaji wenye tija,” amesema mkuu wa wilaya Makilagi.

Aidha ameipongeza OSHA kwa kuwa mstari wa mbele kusaidia makundi mbalimbali ya wahitaji katika jamii wakiwemo Watu wenye Ulemavu kupitia rasimali za taasisi hiyo pamoja na michango ya watumishi na kutoa rai kwa taasisi zingine kuiga mifano wa OSHA.

Akimkaribisha mkuu wa wilaya katika Bonanza, Mtendaji Mkuu wa OSHA Khadija Mwenda, amesema tukio hilo ni utekelezaji wa mikakati wake wa kurudisha kwa jamii na chuo hicho cha mirongo kimepatiwa msaada huo kutokana na kuwa na uhitaji mkubwa wa vifaa vilivyotolewa uliobaishwa na wataalamu wa OSHA baada ya kutembelea chuo hicho hapo awali.

“Tukio hili ni utekelezaji wa mkakati wetu wa kurudisha kwa jamii. Tulitembelea chuo hiki na kubaini mahitaji yao na hivyo kuona ni muhimu kuwawezesha kwa kuwapata vifaa vya msingi vikiwemo  jezi na mipira ambapo awali walikuwa wanalazimika kukodi jezi hizo kila wanaposhiriki MASHINDANO ya kimichezo” ameeleza mkuu huyo wa taasisi ya OSHA na kuongeza:

“Chuo hiki pia kina wanafunzi wenye Ulemavu na sisi tunaamini kwamba Ulemavu ni hali ambayo haipaswi kuwa kikwazo kwa mtu kujiendeleza kiujizi na kushiriki shughuli za kiuchumi hivyo kupitia tukio hili la kimichezo na vifaa tulivyowakabidhi vijana hawa watahamasika kushiriki michezo na hivyo tutaweza kujenga Taifa imara lenye nguvu na lenye umoja

“Kwa upande wao kaimu mkuu wa chuo hicho Herieth Richard na mwanafunzi wa fani ya ushonaji katika chuo hicho Aneth Augustino wamemshukuru OSHA kwa kuwawezesha upatikanaji wa mahitaji yao ya msingi vikiwemo vifaa VYA michezo.

“Tunaishukuru sana taasisi ya OSHA kwa kutuona na kuamua kutupatia msaada wa mahitaji yetu ya muhimu tunatambua kwamba vyuo vyenye mahitaji kama haya ni vingi lakini OSHA wameamua kutuchagua sisi.

Kwa Kweli tunawashukuru sana kwa tendo lao hili la huduma sana kwetu,” ameeleza mkuu wa chuo cha mirongo.Bonanza hilo la OSHA la huduma kwa jamii ( OSHA CSR Bonanza 2025)lilifanyika Sept 17,2025 katika viwanja vya shule ya. Nyakabungo iliyopo katika wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza na kuhusisha timu za OSHA na vyuo vya ufundi vya Mirongo, Nyakato na Kisesa.

Michezo iliyoshindaniwa ni mpira wa miguu wa Pete, riadha, kukimbia kwenye magunia, kukimbia na medium kwenye kijiko, rede na kukamata kuku.Chuo cha mirongo kinafundisha fani za umeme, uselemala, ushonaji na uchomeleaji kinamilikiwa na serikali chini ya Ofisi ya Waziri mkuu ( kazi vijana ajira na watu wenye Ulemavu )