Na Mwandishi wetu,timesmajira
NAIBU Waziri wa Afya Mhe. Dkt. Godwin Mollel amesema, Serikali imetenga shilingi Bilioni 10.7 kwa ajili ya kutekeleza Mpango Mkakati wa Tatu wa Kitaifa wa Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa Yasiyoambukiza.
Dkt. Mollel amesema hayo, wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Mtoni, Idrissa Juma Abdul – Hafar katika kikao cha pili cha Bunge la 9, Jijini Dodoma.
Amesema, Mpango mkakati huo, umeainisha mikakati mahsusi ya udhibiti wa visababishi vya magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo, Kuimarisha uratibu na ushirikishwaji wa sekta mtambuka, kuimarisha miundombinu ya utoaji wa huduma.
Aliendelea kusema kuwa, mipango mingine ni pamoja na kuimarisha uwezo watumishi katika kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiza, kuimarisha na kusimamia shughuli za utafiti pamoja na kuhamasisha wananchi kuhusu njia za kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza, pamoja na kujenga tabia ya kufanya mazoezi.
Aidha, Dkt. Mollel amesema kuwa, Serikali inaendelea kuhamasisha wananchi kujiunga na Bima ya afya kwa wote pindi Sheria hiyo itakapopitishwa na Bunge ili kupunguza gharama za matibabu kwa wananchi, hasa matibabu ya magonjwa yasiyoambukiza.
Sambamba na hilo, Dkt. Mollel amesema Rais wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan ametenga kiasi cha Shilingi Bilioni 149.77 kwaajili ya kuwapatia Bima wananchi wasio na uwezo.
More Stories
Serikali kupeleka mawasiliano maeneo ya mipakaniÂ
Sekondari ya Butata mbioni kufunguliwa Musoma Vijijini
TIC yapongeza mradi wa Kampuni ya Big Best