December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Serikali imepiga vitabu 16 kutumika mashuleni,vinahatarisha malezi ,makuzi ya watoto

Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma

SERIKALI imepiga marufuku vitabu 16 kutumika mashuleni kutokana na vitabu hivyo kukinzana na mila na desturi na tamaduni za kitanzania .

Aidha imesema,kwa shule ambayo itabainika kuendelea kutumia vitabu hivyo mara baada ya katazo la Serikali itachukuliwa hatua mbalimbali za kinidhamu na kisheria ikiwemo kufutiwa usajili wake.

 Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kufutwa kwa vitabu hivyo Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda amesema, uwepo wake pia unahatarisha  malezi bora ya watoto.

Amevitaja vitabu vilivyopigwa marufuku kutumika mashuleni ni pamoja na Diary of Wimpy Kid,Dairy of Wimpy Kid-Rodrick Rules,Diary of Wimpy Kid- The last Straw,Diary ofi Wimpy Kid –The Ugly Truth na Diary of Wimpy Kid-Cabn Fever.

Vitabu vingine vilivyopigwa marufuku hiyo ni Diary of Wimpy Kid –The Third Wheel,Diary of Wimpy Kid –Hard Luck,Diary of Wimpy Kid-The long Haul,Diary of Wimpy Kid –Old SchoolDiary of Wimpy Kid-Double Down na Diary of Wimpy Kid-The Gateway.

Kwa mujibu wa Profesa Mkenda ,pia vitabu vya Diary of Wimpy Kid-Diper Overlode,Is for TANSGENDER(you know best who you are),Is for LGBTQIA (find the word that make you you na Sex Education a guid to life ,vyote vimepigwa marufuku.

“Hii ni orodha ya kwanza ,baada ya ukaguzi na kuhakikiwa kwamba vitabu hivi vinakiuka maudhui ya malezi mema ya mtanzania,ukaguzi unaendelea ,tunahimiza wazazi ,walimu ,wanafunzi na jamii kwa ujumla kwa ambaye atagundua kitabu kingine chochote kinachokiuka maudhui apige simu kwenye namba 0262160270 au 0737962965.”amesema Profesa Mkenda

Waziri huyo ametumia nafsi hiyo kuwahimiza wazazi kukagua mabegi ya watoto mara kwa mara ili kuhakikisha hawatumii vitabu hivyo.