Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma
MTENDAJI Mkuu wa Mfuko wa Utamaduni na Sanaa Tanzania Nyakaho Mahemba amesema Mfuko huo ulianzishwa na Serikali ikiwa ni jitihada za makusudi ya kuanzisha, kukuza na kuendeleza sekta ya utamaduni na sanaa hapa nchini.
Hayo yamesemwa na Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Utamaduni na Sanaa hapa nchini wakati akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma mara baada ya kuhitimishwa bajeti ya Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo kwa mwaka wa Fedha wa 2023/24.
Mtendaji Mkuu huyo amesema lengo kuu la mfukohuo  ni kuinua viwango vya ubora vya kazi za wadau wa utamaduni na sanaa ili  viweze kukidhi mahitaji ya soko la ndani na soko la nje .
“Ili kufikia lemgo hilo mfuko unatoa huduma za mikopo yenye masharti nafuu ambapo kuna mikopo ya vitendea kazi ili kumsaidia msanii kuzalisha kazi bora zitakazokidhi mahitaji ya soko la nje,
Vile vile alisema, ipo mikopo ya uendeshaji na mikopo ya kujikimu kwa ajili ya kazi za nje ya nchi kwa matumizi ya nauli.
Aidha amesema,mikopo inayotolewa ni ile yenye riba nafuu ya asilimia mbili ambayo itamwezesha kila mmoja kumudu marejesho na kuwawezesha wengine kunufaika na huduma hiyo huku akisema, mnufaika anaweza kukopa kiasi cha pesa kuanzia shilingi laki mbili mpaka milioni mia moja,
Amesema,mikopo hiyo inatolewa kwa vikundi hata kwa mtu mmoja mmoja na makampuni.
Mahemba ametumia nafasi hiyo kuwaomba wadau wote na wananchi kwa ujumla kufika ofisi za utamaduni na sanaa kwa ajili ya kupata elimu zaidi juu ya mikopo hiyo .
Aidha ametumia nafasi hiyo kuwaomba  wale wote waliokopeshwa watumie mikopo hiyo vizuri pamoja na kurejesha kwa wakati ili na wengine waweze kunufaika huduma hiyo.
More Stories
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba
TRA kuongeza idadi ya waendesha uchumi walioidhinishwa
TRA Tanga wajivunia ukusanyaji mapato