MADRID, Uhispania
BEKI wa kati katika klabu ya Real Madrid, Sergio Ramos anatarajia kuondoka kwenye klabu hiyo baada ya mkataba wake utakapomalizika mwishoni mwa mwezi, huku mchezaji huyo akiitumikia Madrid takribani miaka 16.
Madrid wamemfanyia sherehe ya kumuaga nahodha wao wa muda mrefu mbele ya rais wa kilabu hiyo Florentino Perez jana sherehe iliyohudhuliwa na watu mbalimbali kutokana na mchango mkubwa wa mchezaji huyo.
Ramos, mwenye umri wa miaka 35 raia wa Uhispania, alitaka mkataba mpya wa miaka miwili kukaa Madrid, lakini vyanzo viliiambia ESPN kwamba Perez hakuwa tayari kuvunja sera yake ya kupeana kandarasi za mwaka mmoja tu kwa wachezaji zaidi ya miaka 30.
Mazungumzo kati ya Perez na Ramos yamekuwa yakiendelea kwa mwaka uliopita na kuendelea hadi Juni. Walakini, hakuna hata mmoja aliyekuwa tayari kuafikiana. Licha ya Ramos hakutaka nyongeza ya mshahara ili abaki Santiago Bernabeu.
Ramos, ambaye alicheza mechi 671 kwa Madrid, akifunga mabao 101, bado hajafanya uamuzi thabiti juu ya maisha yake ya baadaye na hakutangaza marudio yake katika hafla hiyo ya kuagana.
Hata hivyo, kocha wa Man City Pep Guardiola, anathamini uzoefu ambao Romos anao na angeongeza uimara kwenye kikosi chake na ushindani ungekuwepo kutokana na mwongozo atakaotoa kwa mabeki wa kati vijana Ruben Dias na John Stones.
More Stories
Watumishi wa Fahari wafanya Bonanza
Rais Samia atia mkono mchezo wa masumbwi Tanzania
Chino bingwa mpya wa IBA Intercontinental Championship